?>

White House: Biden kugombea katika uchaguzi wa rais Marekani mwaka 2024

White House: Biden kugombea katika uchaguzi wa rais Marekani mwaka 2024

Msemaji wa White House ametangaza kuwa Joe Biden rais mwenye umri mkubwa zaidi wa Marekani ambaye katika miezi ya karibuni amepoteza umashuhuri wake kwa kiasi kikubwa ana mpango wa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka 2024 nchini humo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, Biden na washauri wake katika siku za karibuni wamekuwa wakihangaika kuwahakikishia waitifaki wa rais huyo kuhusu uamuzi wake wa kushiriki katika duru ya pili ya urais huko Marekani. Ripoti hii imechapishwa baada ya jarida la wiki iliyopita la Politoco kutoa ripoti kuhusu machaguo mengine ya wagombea wanaoweza kuwania kiti cha urasia kutoka chama cha Democrat iwapo Biden hatogombea tena kiti hicho. 

Katika hali ambayo ripoti zinasema kuwa Rais Joe Biden huenda katika miaka miwili ijayo akabadili mipango yake kwa ajili ya mwaka 2024; duru zilizo karibu na rais huyo zilisisitiza tangu Biden aingie madarakani mwezi Januari kwamba atagombea duru ya pili ya urais nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, tetesi zinazoendelea kuhusu iwapo Biden atawania tena kiti cha urais au la kutokana na umri wake mkubwa na kupungua uungaji mkono wa wananchi kwa rais huyo zimeongezeka na kupata nguvu katika wiki za karibuni. Wakati huo huo chunguzi za maoni zilizofanywa siku kadhaa zilizopita zinaonyesha kupungua kwa kasi uungaji mkono wa wananchi kwa Rais Joe Biden kutokana na hali ya kiuchumi ilivyo sasa nchini Marekani khususan kuongezeka bei za bidhaa mbalimbali nchini. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*