?>

WHO: Aghalabu ya nchi duniani hazina chanjo ya corona kwa ajili ya wahudumu wa afya

WHO: Aghalabu ya nchi duniani hazina chanjo ya corona kwa ajili ya wahudumu wa afya

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la afya Duniani (WHO) amesema kuwa, si sahihi kwa nchi tajiri kuagiza chanjo za ziada wakati aghalabu ya nchi duniani bado hazijapokea chanjo ya corona.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Dakta Tedros Adhanom Gebreyesus amesema kuwa, vifo vinavyotokana na corona vinaongezeka, na kwamba spishi ya kirusi cha corona aina ya Delta inaendelea kubadilika na aghalabu ya nchi duniani bado hazijapokea chanjo za kutosha za corona kwa ajili ya kuwalinda wafanyakazi wa sekta ya afya na tiba. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani ameeleza kuwa, kuna pengo kubwa duniani katika uandaaji wa chanjo ya corona. Baadhi ya nchi na maeneo duniani yanaagiza chanjo za corona za ziada huku nchi nyingine zikisalia bila ya suhula muhimu zinazohitajika kwa ajili ya kuwapatia chanjo wafanyakazi wa sekta ya afya na tiba katika nchi hizo. 

Afisa huyo wa Shirika la Afya Duniani ameashiria makampuni ya Kimarekani yanayozalisha chanjo ikiwemo chanjo ya Pfizer na kueleza kuwa, makampuni hayo yanapasa kutuma dozi za chanjo ya corona kwa mpango wa COVAX hususan kwa nchi zenye watu maskini na wenye kipato cha wastani.

Dakta Adhanom amebainisha hayo huku Shirika la Afya Duniani likituhumiwa kuwa halikuchukua hatua za kutosha za kugawa chanjo ya corona katika baadhi ya maeneo duniani.  

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela aliwahi kulituhumu shirika la WHO kuwa limekwamisha operesheni ya kutumwa chanjo ya corona kwa wakati nchini humo licha ya kupokea fedha za manunuzi.

Hadi sasa watu zaidi ya milioni 188 wameambukizwa corona kote duniani na zaidi ya milioni nne na 57 elfu  wameaga dunia kwa ugonjwa huo. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*