?>

WHO: Huenda watu laki 5 zaidi watakufa kwa Corona Ulaya

WHO: Huenda watu laki 5 zaidi watakufa kwa Corona Ulaya

Shirika la Afya Dunia (WHO) limetahadharisha kuwa, yumkini watu laki tano wakapoteza maisha katika nchi za Ulaya kutokana na ugonjwa wa COVID-19 kufikia mwezi Machi mwaka ujao, iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Dakta Hans Kluge, Mkurugenzi wa WHO barani Ulaya amesema shirika hilo linatiwa wasiwasi na wimbi jipya la maabukizi ya ugonjwa huo katika nchi za Ulaya, jambo ambalo limezilazimisha nchi nyingi barani humo kutangaza upya hatua kali za kudhibiti msambao huo, ikiwemo kufunga nchi.

Dakta Kluge amesema kuwadia msimu wa baridi kali ambao kimsingi hushadidisha maambukizi ya virusi na vile vile kiwango cha chini ya utoaji chanjo ya kupambana na Corona ni miongoni mwa mambo yaliyopelekea kushuhudiwa ongezeko la sasa la vifo na kesi za ugonjwa huo huko Ulaya.

Hivi karibuni, Shirika la Afya Dunia (WHO) lilionya kuwa, vifo na kesi za Corona zinapungua katika maeneo yote duniani isipokuwa katika nchi za bara Ulaya.

Ongezeko hilo la kuogofya la vifo na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 linaripotiwa katika nchi za Ulaya katika hali ambayo, nchi hizo zinaongoza duniani kwa idadi ya watu waliopiga chanjo za kukabiliana na maradhi hayo.342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*