?>

WHO: Kutozingatia masharti na kushindwa kuchukua hatua mapema, sababu kuu ya 'tsunami' ya corona nchini India

WHO: Kutozingatia masharti na kushindwa kuchukua hatua mapema, sababu kuu ya 'tsunami' ya corona nchini India

Shirika la Afya Duniani WHO limesema kuwa, janga la corona au COVID-19 limeendelea kuwa jinamizi kwa India ambapo kila siku linaongeza idadi ya wagonjwa wapya kati ya 350,000 na 400,000 huku wengine kwa maelfu wakipoteza maisha kila leo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Takwimu za shirika hilo zinaonyesha kwamba karibu watu 220,000 wameshapoteza maisha hadi sasa kwa COVID-19 nchini India huku wagonjwa waliothibitishwa kukumbwa na ugonjwa huo hadi hivi sasa wakipindukia milioni 20.

Idadi rasmi ya wagonjwa wa corona waliotangazwa na serikali ya India hadi leo mchana walikuwa ni milioni 20 na laki 2 na 82,833.

Wataalamu wa mambo wanadadisi kwa kusema: Ni nini kilichochangia hali kufikia pabaya kiasi hiki, mfumo wa afya kulemewa kupita kiasi, vitanda kufurika mahospitali, uhaba mkubwa wa dawa na hewa ya oksijeni na hata upungufu wa wahudumu wa afya?

Anshu Sharma, mwandishi wa habari wa Umoja wa Mataifa nchini India amezungumza na mkuu wa WHO nchini humo Dk. Roderico H. Ofrin ambaye amesema:  “Nadhani ni muhimu kutambua kwamba mwezi kama wa Februari hivi maisha yalirejea katika hali ya kawaida, shughuli za kiuchumi na kijamii zikaanza kuendendelea kama kawaida, lakini pia tumeshuhudia watu kutozingatia masharti ya kukabiliana na COVID-19 na hayo yamekipa kirusi cha corona, fursa na fasi za kuendelea kusambaa. Ingawa kuna sababu nyingi lakini kubwa ni kwamba tumekipa kirusi hiki fursa ya kuendelea kuambukiza.” 

Baada ya Marekani ambayo imetangaza kuwa na wagonjwa milioni 33 na 230,992 wa corona, India sasa imeshika nafasi ya pili na kuipiku hata Brazil. 

Alipoulizwa nini cha kufanya ili kuikoa India na janga hili ambalo limetajwa pia kwa jina la "tsunami ya corona," Dk. Ofrin amesema, ni muhimu hatua zote zikaendelea kuzingatiwa ikiwemo kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, umbali kati ya mtu na mtu, upimaji.

Zaidi ya hayo amesema: “Kuna nyenzo nyingine ya kulikabili janga hili ambayo ni chanjo. India imeweza kutoa chanjo kwa watu milioni 165 hadi sasa . Hii ni njia nyingine ambayo kwa hakika itasaidia kukomesha maambukizi ya mripuko huu wa pili - kama wanavyouita - wa COVID-19.” 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*