?>

WHO: Muda si mrefu nusu ya wakazi wa Ulaya wataambukizwa Omicron

WHO: Muda si mrefu nusu ya wakazi wa Ulaya wataambukizwa Omicron

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, nusu ya bara Ulaya itakuwa imeambukizwa kirusi cha Covid -19 aina Omicron ndani ya wiki sita hadi nane zijazo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Dk Hans Kluge Mkurugenzi Mtendaji wa WHO barani Ulaya amesema hayo akinukuu taasisi moja ya takwimu na tathmini ya afya iliyosema kwamba, zaidi ya asilimia 50 ya wakazi wa Ulaya wataambukizwa Omicron katika muda wa wiki sita hadi nane zijazo".

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani idadi ya maambukizi ya virusio vya Corona barani Ulaya imeongezeka zaidi ya mara mbili katika kipindi cha wiki mbili.

Uchunguzi wa hivi majuzi unaonyesha kuwa, spishi mpya ya Corona ya Omicron ina uwezekano mdogo wa kuwafanya watu kuwa wagonjwa sana kuliko aina nyingine za awali za Covid-19. Lakini Omicron bado inaambukiza sana na inaweza kuwaambukiza watu hata kama wamechanjwa kikamilifu.

Siku ya Jumatatu, Uingereza iliripoti kesi zaidi 142,224 zilizothibitishwa za virusi hivyo na vifo 77. Hospitali kadhaa zimetangaza matukio "muhimu" kwa sababu ya kutokuwepo kwa wafanyakazi na shinikizo linalosababishwa na Covid-19.

Kwingineko, idadi ya wanaolazwa hospitali pia inaongezeka. Waziri wa Afya wa Ufaransa Olivier Veran alionya wiki iliyopita kwamba Januari itakuwa ngumu kwa hospitali.

Huko Ulaya mashariki, Poland iliripoti kuwa watu 100,000 walikuwa wamekufa kutokana na virusi nchini tangu kuanza kwa janga hilo. Poland sasa ina kiwango cha sita cha vifo vya juu zaidi ulimwenguni kutokana na Covid-19, na karibu 40% ya watu wake bado hawajachanjwa.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*