?>

Wizara ya Mambo ya Nje: Usafirishaji wa bidhaa za Iran Afrika umeongezeka kwa 120%

Wizara ya Mambo ya Nje: Usafirishaji wa bidhaa za Iran Afrika umeongezeka kwa 120%

Mkuu wa Idara ya Magharibi na Katikati mwa Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, usafirishaji wa bidhaa kuelekea nchi za bara la Afrika umeongezeka kwa asilimia 120.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kabla ya hapo, Farzad Piltan Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Nchi za Kiarabu na Kiafrika ya Shirika la Maendeleo ya Biashara la Iran alitangaza kuwa, usafirishaji bidhaa kuelekea nchi za Afrika umevunja rekodi na kufafanua kwamba, katika mwaka uliopita wa 1400 Hijria Shamsia, usafirishaji wa bidhaa za Iran kuelekea nchi za Afrika uliongezeka kwa asilimia 107 na kufikia dola milioni 1,195.

Kwa mujibu wa Idara ya Uhusiano wa Umma ya Chama cha Biashara, Viwanda, Madini na Kilimo cha mkoa wa Alborz, Ali Akbar Rezai Mkuu wa Idara ya Magharibi na Katikati mwa Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: usafirishaji bidhaa za Iran kuelekea nchi za bara la Afrika katika mwaka uliopita wa 1400 uliongezeka kwa asilimia 120 kulinganisha na mwaka wa kabla yake na kufikia dola bilioni moja na milioni 200.

Akihutubia semina ya kujadili soko la nchi ya Senegal iliyofanyika kwa njia ya intaneti kwa kuhudhuriwa na balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo na wawakilishi kadhaa wa sekta za viwanda wa mkoa wa Alborz, Rezai ameongeza kuwa, Afrika Magharibi ina idadi ya watu wanaokaribia milioni 400 na ni eneo lenye idadi mwafaka ya watu kwa ajili ya uwekezaji na usafirishaji bidhaa za Iran.

Halikadhalika, Mkuu wa Idara ya Magharibi na Katikati mwa Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kuna nchi zaidi ya 20 katika eneo la magharibi mwa Afrika zikiwemo Senegal, Ghana, Ivory Coast, Nigeria, Mali na Guinea, ambazo zina uwezo na fursa nzuri kwa ajili ya mahusiano ya kibiashara.../342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*