?>

Yemen: Ikiwa UAE itaendeleza uadui, tutaishambulia hadi ndani kabisa ya ardhi yake

Yemen: Ikiwa UAE itaendeleza uadui, tutaishambulia hadi ndani kabisa ya ardhi yake

Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen ameionya Imarati (UAE) kuwa, endapo itaendeleza uadui, vikosi vyao vya serikali ya uwokovu wa kitaifa vitashambulia hadi maeneo ya ndani kabisa ya ardhi ya nchi hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Muhammad al Bukhaiti ametoa onyo hilo baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kushadidisha hatua za kiuadui katika maeneo ya kusini mwa Yemen.

Al Bukhaiti amesema, kuna muamala unaofanywa kati ya Saudi Arabia na Imarati, ambao ni wa utawala wa Aal Saudi kuikabidhi Imarati mikoa yote ya kusini mwa Yemen ukiwemo wa Shabwah; na mkabala wake, kama ilivyokuwa hapo kabla, Imarati itatumia nguvu na uwezo wote wa kijeshi nchini Yemen kwa ajili ya Saudia.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen ameongezea kwa kusema: "Kutokea hapa, ninaiasa Imarati isiendeleze hatua zake za kuchochea mivutano, kwa sababu, kama mivutano hii itaendelea, Yemen italazimika kushambulia hadi ndani kabisa ya ardhi ya Imarati."

Muhammad al Bukhaiti amesisitiza kuhusu uwezekano wa kurudiwa tena shambulio la makombora lililowahi kufanywa huko nyuma hadi ndani ya ardhi ya umoja huo wa falme za Kiarabu na akasema: "Sisi tuko kwenye hali ya vita".

Kwa muda sasa, mapigano makali yanaendelea katika mkoa wa Shabwah kusini mwa Yemen kati ya mamluki wa Imarati na vikosi vya jeshi la Yemen vikishirikiana na vya wapiganaji wa kujitolea vya wananchi wa nchi hiyo. Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, vikosi vya Yemen vimetungua ndege mbili zisizo na rubani za ujasusi za Imarati, wakati zilipokuwa kwenye operesheni ya kiuadui kusini mwa nchi hiyo.

Hivi karibuni pia, na katika hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa katika vita vya Yemen, kikosi cha wanamaji cha nchi hiyo kimeinasa na kuiteka meli ya Imarati iliyokuwa imebeba shehena ya silaha na zana za kijeshi kwa ajili muungano vamizi wa kijeshi wa Saudia katika maji ya magharibi mwa nchi hiyo.../342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*