?>

Zarif alaani unafiki wa Marekani na Ulaya kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA

Zarif alaani unafiki wa Marekani na Ulaya kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Marekani na Ulaya zinafanya unafiki katika mienendo yao kuhusiana na makubalino ya nyuklia ya Iran maarufu kwa kifupi kama JCPOA.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Muhammad Javad Zarif amesema kuwa Ulaya imeeleza wasiwasi wake kuhusiana na miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia ya Iran na huu kwa hakika ni unafiki na msimamo wa kindumakwili. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesemea kuwa Marekani inatoa adhabu kwa upande wowote unaokataa kutekeleza sheria zake lakini wakati huo huo inakataa kutekeleza ahadi na majukumu yake. Ameongeza kuwa, siasa za Marekani hazijabadilika, na rais wa nchi hiyo Joe Biden anatoa madai matupu.

Javad Zarif amesisitiza kuwa, Marekani haitaweza kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kabla ya kuondoa viwazo vyote dhidi ya Iran kwa sababu nchi hiyo ndiyo liyokiuka na kukanyaga sheria.

Katika upande mwingine Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa utawala haramu wa Israel unapanua zaidi kituo cha nyuklia cha Dimona ambacho ndicho kituo pekee kinachotengeneza mabomu ya nyuklia katika eneo la Mashariki ya Kati lakini hadi sasa hatujaona tangazo la kuwa na wasiwasi kutoka nchi za Magharibi.

Zarif ameashiria fatuwa iliyotolewsa na Ayatullah Ali Khamenei akiharamisha utengenezaji wa mabomu ya nyuklia na kuongeza kuwa, tunayo fatuwa inayoharamisha kumiliki na kuunda silaha za nyuklia.

Vilevile ameashiria mazungumzo yake na Mkurugenzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, Rafael Grossi hapa nchini Iran na kusema wakala huo unapaswa kuwa na mienendo ya kimantiki.

Zarif amesema Iran haina mpango wa kuunda silaha za nyuklia na nchi za Ulaya zinapaswa kuwa na mienendo sahihi katika masuala ya kiuchumi.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni