?>

Zarif: Hatua ya Marekani dhidi ya Ansarullah ni dharau kwa amani

Zarif: Hatua ya Marekani dhidi ya Ansarullah ni dharau kwa amani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amelaani vikali hatua ya utawala unaoondoka madarakani Marekani dhidi ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika ujumbe wa Twitter siku ya Ijumaa, Zarif amesema uamuzi wa Marekani wa kuiweka Harakati ya Ansarullah ya Yemen katika orodha yake ya makundi ya 'kigaidi' ni dhihirisho la namna Marekani inavyodharau amani.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alitangaza kuiweka Harakati ya Ansarullah katika orodha ya Washington ya makundi ambayo inayataja kuwa ya kigaidi. Aidha viongozi watatu wa kundi hilo pia wamewekwa katika orodha ya Marekani ya 'magaidi wa kimataifa'. Uamuzi huo utaanza kutekelezeka Januari 19, siku moja tu kabla ya utawala wa Donald Trump kuondoka madarakani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika ujumbe wake wa Twitter ameandika: "Katika siku zake za mwisho zilizojaa fedheha, Pompeo ameonyesha dharau kwa amani kufuatia uamuzi  dhidi ya Ansarullah na kueneza ngoma za kivita na urongo dhidi ya Iran." Zarif amesema hatua  dhidi ya Ansarullah itafanya hali ya kibinaadamu kuwa mbaya zaidi nchini Yemen.  Hali kadhalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria maamuzi mengi yaliyo dhidi ya ubinadamu ambayo yamechukuliwa na utawala wa Trump katika kipindi cha miaka minne iliyopita na kusema: "Inaonekana uharibifu uliosababishwa na utawala wa Trump dhidi ya ubinadamu hautoshi kwa watu wenye misimamo mikali katika utawala huo."

Uamuzi wa Marekani wa kuitangaza Ansarullah kuwa eti ni kundi la kigaidi umelaaniwa pia na Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.

David Beasley Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani (WFP) amesema kuwa uamuzi wa Marekani dhidi ya harakati ya Ansarullah ya Yemen ni sawa na kutolewa hukumu ya kifo kwa Wayemen wasio na hatia. Naye Martin Griffiths, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Yemen amesema kuliweka kundi la Ansarullah katika orodha ya makundi ya kigaidi kutaeneza njaa huko Yemen na kufanya kuwa ngumu zaidi shughuli za mashirika ya ufikishaji misaada ya kibidamu nchini humo. 

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*