?>

Zarif: Marekani inapaswa kuondoa bila masharti yoyote vikwazo vyote vilivyowekwa na Trump

Zarif: Marekani inapaswa kuondoa bila masharti yoyote vikwazo vyote vilivyowekwa na Trump

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Marekani inapaswa kuondoa bila masharti yoyote na kwa namna iliyo athirifu vikwazo vyote vilivyorejeshwa upya na kutekelezwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Donald Trump.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mohammad Javad Zarif ametoa sisitizo hilo leo katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa kijamii wa twitter, likiwa ni jibu kwa hatua ya Marekani ya kulegeza msimamo kwa kufuta uamuzi wake wa kutekeleza kanuni ya kurejesha kwa mpigo vikwazo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran. 

Amesema: "Marekani imekiri kuwa madai ya Pompeo kuhusu azimio 2231 hayana itibari yoyote kisheria; na sisi tunaafiki."

Dakta Zarif ameongeza kuwa, katika kuheshimu na kutekeleza azimio 2231, Marekani inapaswa kuondoa bila masharti yoyote na kwa namna iliyo athirifu vikwazo vyote vilivyorejeshwa upya na kutekelezwa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Donald Trump.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, baada ya kuondolewa vikwazo na Marekani, Iran nayo itarejesha haraka katika hali yake ya awali hatua zote rekebishi (za kupunguza uwajibikaji katika JCPOA) ilizokuwa imechukua.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni