?>

Zarif: Vikwazo havijawa na athari kwa maendeleo ya nyuklia ya Iran

Zarif: Vikwazo havijawa na athari kwa maendeleo ya nyuklia ya Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemshauri rais wa Marekani aangalie takwimu na tarakimu zinazoonyesha kuwa vikwazo havijawa na athari kwa upigaji hatua za maendeleo Iran katika sekta ya nyuklia.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mohammad Javad Zarif amesema hayo katika ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa sita tangu yaliposainiwa makubaliano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na kubainisha kuwa, miaka sita iliyopita katika siku kama hii JCPOA ilitatua maudhui inayohusiana na Sura ya Saba ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pasi na kutumia vita.

Zarif ameendelea kuandika katika ujumbe wake huo kwamba, Barack Obama (rais wa wakati huo wa Marekani) alibaini kuwa "vikwazo vyake vya kulemaza" haviwezi kuilemaza Iran wala mashinepewa (centrifuges) za Iran.

Katika sehemu nyingine ya ujumbe wake huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika: aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump alidhani kwa mawazo yake "mashinikizo ya juu kabisa" yatawezesha kufikiwa lengo hilo lakini haikuwa hivyo katu.

Dakta Zarif amesisitiza kuwa: rais wa sasa wa Marekani Joe Biden inapasa aziangalie kwa makini takwimu na tarakimu hizi.

Katika ujumbe wake huo aliotuma kwenye mtandao wa intaneti, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameweka taswira ya takwimu na tarakimu zinazohusu vikwazo vya Marekani na maendeleo iliyopata Iran katika mpango wake wa nyuklia ambazo zinaonyesha kuwa vikwazo hivyo havijawa na athari kwa maendeleo ya Iran.../

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*