?>

Zoezi la kumimina maji kwa awamu ya pili katika Bwawa la al Nahdha lamalizika

Zoezi la kumimina maji kwa awamu ya pili katika Bwawa la al Nahdha lamalizika

Licha ya kuweko maonyo na vitisho vikali vya Sudan na Misri, lakini duru moja ya masuala ya umwagiliaji maji nchini Ethiopia imesema kuwa, zoezi la kumimina maji kwa awamu ya pili katika Bwawa la al Nahdha limekamilika.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kumalizika awamu ya pili ya kumimina maji katika Bwawa la al Nahdha nchini Ethiopia kumetangazwa katika hali ambayo, wabunge wa Misri wamelalamikia kuhusika utawala wa Kizayuni wa Israel katika mzozo wa bwawa hilo baina ya Ethiopia, Misri na Sudan.

Mbunge mmoja wa Misri amefichua kuwa, Bwawa la al Nahdha ni mgogoro wa kisiasa na lengo lake hasa ni kuhakikisha maji ya Mto Nile yanaunufaisha utawala wa Kizayuni wa Israel.

Seiku chache zilizopita, serikali ya Ethiopia ilianza zoezi la kumimina maji kwa awamu ya pili katika Bwawa la al Nahdha bila ya kujali kukubali au kukataa nchi mbili za Misri za Sudan zilizolalamikia vikali zoezi hilo.

Shirika la habari la IRIB liliripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, katika hali ambayo viongozi wa Misri na Sudan wanaendelea na mazungumzo ya kuizuia Ethiopia isiingize maji kwa awamu ya pili katika Bwawa la al Nahdha, viongozi wa Addis Ababa wameamua kufanya zoezi la kumimina maji kwenye bwawa hilo bila ya kujali kupinga au kukataa nchi mbili za Misri na Sudan.

Misri na Sudan zimeipokea kwa hasira hatua hiyo ya Ethiopia na zinaendelea na harakati zao za kukabiliana na matumizi ya Bwawa la al Nahdha. Sudan na Misri zinaamini kuwa hilo litatumia maji mengi ya Mto Nile na hiyo ina maana ya kutangaza mauaji ya umati kwa wananchi wa Sudan na Misri.

342/


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*