-
Iran yaendelea kumiliki ujuzi wa ujenzi wa Mitambo ya Nyuklia
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema kuwa Marekani imeshindwa kuzuia ujenzi wa mtambo wa nyuklia wa Karun katika jiji la Darkhovein, kusini magharibi mwa Iran, akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu inaendelea kufuatilia shughuli zake za nyuklia kwa amani licha ya njama za maadui.
-
Iran inauza zana zake za kijeshi katika nchi 30
Waziri wa Ulinzi wa Iran, Meja Jenerali Aziz Nasirzadeh, ametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa inauza vifaa vya kijeshi kwa nchi 30 duniani.
-
Kilele cha utayarifu wa Jeshi la Iran kwa ajili ya kukabiliana na tishio la adui
Pembezoni mwa hatua ya mwisho ya mazoezi ya kijeshi yaliyopewa jina la Mtume Mtukufu wa 19 (SAW) ya Vikosi vya Jeshi la Nchi Kavu vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Meja Jenerali Mohammad Bagheri, Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu viko katika kilele cha utayarifu.
-
Jeshi la Iran laanza Luteka ya Zulfiqar-1403 pwani ya kusini
Vikosi tofauti vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimeanza awamu kuu ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya Zulfiqar-1403 leo Jumamosi (Februari 22) katika pwani ya Makran, kusini mashariki, Bahari ya Oman, na kaskazini mwa Bahari ya Hindi.
-
Iran: Tutajikita katika kuimarisha uhusiano na mataifa ya Afrika
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imesisitiza kuwa, irada ya Jamhuri ya Kiislamu imeelekezwa katika kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya Afrika.
-
Kiongozi Muadhamu: Maandamano dhidi ya Israel yanaashiria kuungwa mkono zaidi Palestina duniani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema maandamano na mikusanyiko dhidi ya Israel barani Ulaya na Marekani inaashiria kuongezeka mshikamano wa kimataifa na taifa la Palestina.
-
Mwana wa Nasrullah asema siku ya Jumapili ya mazishi ya baba yake ni "Siku ya Kutangaza Msimamo"
Sayyid Muhammad Mahdi Nasrullah, mwana wa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon aliyeuawa shahidi amesema katika hotuba ya kuwatolea mwito watu kuhudhuria mazishi ya baba yake kwamba: "kushiriki katika mazishi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah kutakuwa ni kushiriki mtu katika siku ya kutangaza msimamo na kudhihirisha kivitendo mapenzi yake kwa Shahidi Nasrullah".
-
EU yamkingia kifua Zelensky baada ya kushambuliwa vikali na Trump
Mvutano kati ya Ulaya na Marekani umeendelea kushtadi, baada ya viongozi wa nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya kumkingia kifua Rais Vladimir Zelensky wa Ukraine, aliyeshambulia kwa maneno makali na Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni.
-
Trump asisitiza tena kuigeuza Canada jimbo la 51 na kuzipora Greenland na Mfereji wa Panama
Rais Donald Trump wa Marekani amesisitiza tena juu ya nia yake ya kuiunganisha Canada na Marekani na kuifanya jimbo la 51 la nchi hiyo, pamoja na azma yake ya kulinyakua eneo la Greenland na Mfereji wa Panama.
-
Kwa nini nchi za Ulaya zitashindwa tu katika kamari na Trump
Kikao cha viongozi wa nchi kadhaa za Ulaya ambacho kilifanyika hivi karibuni huko Paris kuhusu mgogoro wa Ukraine kilimalizika bila natija yoyote.
-
Ripoti ya Human Rights Watch yafichua jinai ya kutisha ya Israel
Shirika la haki za binadamu la Humar Rights Watch limetoa ripoti mpya inayoonesha ukatili na jinai kubwa ya kuchupa mipaka iliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza.
-
Askofu Mkuu wa Quds: Palestina, kamwe haitomsahau Nasrullah
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ugiriki katika mji mtukufu wa al-Quds unaokaliwa kwa mabavu, Atallah Hanna, amemuenzi na kumsifu aliyekuwa Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah nchini Lebanon, Sayyid Hassan Nasralluh, akisisitiza kuwa watu wa Palestina daima wataendelea kuwa waaminifu kwake kwa namna alivyojitolea muhanga.
-
Netanyahu adai mabaki ya mwili yaliyorejeshwa si ya Shiri Bibas, HAMAS yamjibu
Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amedai kuwa harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imekiuka masharti ya makubaliano ya kubadilishana mateka kwa sababu imekabidhi mwili wa mwanamke asiyejulikana kutoka Ghaza badala ya ule wa mateka wa Kizayuni Shiri Bibas.
-
Mateka wa Kizayuni: Kwa muda wote walipotushikilia, Al-Qassam waliamiliana nasi kwa wema
Gazeti moja la Kizayuni limemnukuu mateka mmoja Muisrael akisema kuwa Wanamuqawama wa Brigedi za al-Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya HAMAS waliamiliana kwa wema na mateka hao wa Kizayuni kwa muda wote walipokuwa wakiwashikilia huko Ukanda wa Ghaza.
-
IAEA: Tumekubaliana na Iran tuendeleze falsafa ya mapatano ya JCPOA
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesema katika mazungumzo na waandishi wa habari mjini Tokyo Japan kuwa: "Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwamba "falsafa ya JCPOA" ambayo msingi wake ni "kuchukua Iran hatua za hiari mkabala wa kupewa upendeleo na motisha," inaweza kuendelea.
-
Iran: Iwapo usalama wetu utahatarishwa, mchokozi hatobaki salama
Mkuu wa Majeshi ya Iran amesema: Iwapo usalama wa taifa letu utahatarishwa, basi usalama wa eneo hili zima la Kusini Magharibi mwa Asia, wahusika wa uchokozi huo na waungaji mkono wao utavurugwa na hawatobaki salama.
-
Salami: Njama za US, Israel kudhuru Muqawama zimegonga mwamba
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Meja Jenerali Hossein Salami amesema, hakuna shaka kwamba juhudi za Marekani na utawala wa Kizayuni za kujaribu kuudhuru mrengo wa Muqawama zitafeli na kugonga mwamba.
-
Rais Pezeshkian: Iran iko tayari kufanya mazungumzo, lakini si "kwa gharama yoyote"
Rais Masoud Pezeshkian amesema Iran imeshatangaza mara kadhaa kwamba iko tayari kufanya mazungumzo lakini haitafanya mazungumzo "kwa gharama yoyote ile".
-
Matakwa ya mashirika ya haki za binadamu ya kutopatiwa Israel vipuri vya ndege za kivita za F-35
Muungano wa Kimataifa wa mashirika 232 ya kutetea haki za binadamu umezitaka nchi mbalimbali zinazohusika katika uundaji za ndege za kivita aina ya F-35 kuacha kuipatia Israel vipuri vya ndege hizo.
-
Abutorabi-Fard: Sayyid Hassan Nasrallah aliuletea Umma wa Kiislamu heshima
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amezungumzia mazishi yajayo ya shahidi Sayyid Hassan Nasrallah na kusema: "Alikuwa mtu mwenye heshima na aliuletea umma wa Kiislamu heshima. Alikuwa shakhsia mashuhuri ambaye alikuwa nafasi muhimu katika kuondoa migogoro."
-
Wabunge EU: Ulaya haiwezi kuendelea kuitegemea Marekani
Wabunge wa Bunge la Ulaya wamesema bara hilo haliwezi kuendelea kuitegemea kikamilifu Marekani kwa ulinzi; na kutoa wito wa kuimarisha uwezo wa kiulinzi wa Ulaya sambamba na kuendelea kuiunga mkono Ukraine.
-
Hatima ya ajabu ya maiti ya mtu aliyechoma moto Qur'ani nchini Sweden!
Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa mwili wa Salwan Momika, aliyechoma moto nakala kadhaa za kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, Qur'ani, ulichomwa baada ya ndugu zake kukataa kupokea mwili wake.
-
Euro-Med: Israel inatumia drone kuwatia hofu watu wa Gaza, inawatisha kwa 'Nakba ya 2, ya 3'
Shirika la kutetea haki za binadamu la Euro-Mediterranean Human Rights Monitor limeonya kuwa utawala wa Kizayunii wa Israel unatumia ndege zisizo na rubani kama silaha ya kisaikolojia kuwatia hofu na wahka Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na hivyo kuzidisha mashinikizo kwa wakazi wa eneo hilo ili wakubali mpango wa Marekani na Israel unaowalazimisha kuhama makazi yao.
-
Oxfam: Tunaanza kuelewa kina cha uharibifu uliofanyika Gaza
Shirika la Oxfam la Uingereza limetangaza kuwa utawala wa Israel umeharibu zaidi ya asilimia 80 ya mitandao ya maji na maji taka ya Gaza na kusababisha hali mbaya ya kiafya.
-
Hamas: Israel iliua mateka wake kwa kulipua vituo walikokuwa wamezuiliwa
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema leo Alkhamisi kwamba, tawi lake la kiijeshi Izuddin al Qassam na muqawama kwa ujumla vina wamefanya kila liwezekanalo kulinda heshima ya maiti wakati wa shughuli ya kukabidhi miili ya matekka hao, ilhali utawala vamizi wa Isarel haukuheshimu uhai yao walipokuwa hai.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Kupanua uhusiano na majirani ni sera ya uhakika ya Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: kupanua uhusiano na majirani ni sera ya uhakika ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Ziyad al-Nakhala: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni egemeo la makundi ya muqawama
Ziyad Al-Nakhala, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni egemeo na muungaji mkono wa makundi ya muqawama.
-
Spika wa Bunge la Iran: Jinai za Israel Gaza na Lebanon ni mauaji ya kimbari
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, jinai za utawala ghasibu wa Israel Gaza na Lebanon ni mauaji ya kimbari.
-
Kwa nini Iran inakaribisha kuimarisha na kupanua uhusiano na nchi jirani?
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Russia, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Azerbaijan, Waziri Mkuu wa Tajikistan na Naibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Turkmenistan. Mazungumzo haya yamefanyika pambizoni mwa Mkutano wa Tatu wa Kiuchumi wa Eneo la Kaspi hapa mjini Tehran.
-
Mwanadiplomasia wa Iran: Marekani, Israel zinajua vyema uwezo halisi wa Iran
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kisiasa, Majid Takht Ravanchi amesema Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zitalazimika kulipa gharama kubwa iwapo zitafanya makosa yoyote dhidi ya Iran.