-
Iran yazindua Jukwaa la Kitaifa la AI: Hatua kubwa kuelekea kwenye kilele cha teknolojia
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua Jukwaa lake la Kitaifa la Akili Mnemba (AI), lililoundwa na watafiti 100 wa Iran, ikiwa ni ishara ya hatua kubwa katika harakati za nchi hii za kujiendeleza na kujitosheleza kiteknolojia.
-
Wanawake wa Iran wanastawi kwa kasi licha ya vikwazo
Licha ya vikwazo, wanawake wa Iran wanaendelea kuwa na azma thabiti ya kujenga mustakabali wa haki zaidi.
-
Araqchi: Iran iko tayari kuzungumza na Ulaya katika mazingira ya kuheshimiana
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Tehran iko tayari kuzungumza na nchi za Ulaya katika mazingira ya kuheshimiana na yanayojali maslahi ya pamoja.
-
Iran: Marekani haina haki ya kutupangia tufuate siasa gani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe akisisitiza kuwa, Marekani haina haki ya kutupangia tufuate siasa gani za kigeni.
-
Salami: Tishio lolote dhidi ya Iran litakabiliwa na jibu la kuumiza
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kwamba, Iran itatoa jibu la maangamivu kwa tishio lolote iwapo litatekelezwa kivitendo dhidi ya taifa hili.
-
Darul-Qur'an yafunguliwa Arusha
Kwa mujibu wa ripoti ta Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA -: Leo hii tarehe 16 Machi, 2025, Taasisi ya Sayyid al-Shuhadaa Jijini Arusha, Tanzania, imezindua Kituo muhimu cha Qur'an Tukufu katika maeneo ya Ngarinaro.
-
Video | Upangaji wa maua kwenye Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s) katika Masiku ya Kuzaliwa kwa Imam Hassan al-Mujtaba (a.s)
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna- Haram Tukufu ya Amir al-Muuminin Ali (a.s) imepambwa kwa maua mazuri katika mnasaba wa Siku ya Kuzaliwa kwa Imam Hassan al-Mujtaba (a.s).
-
Somalia na Sudan zimekataa ombi la kuwapa makazi Wapalestina wanaoishi Gaza
Mamlaka za nchi mbili, Somalia na Sudan, zimekataa katakata pendekezo na mpango wowote kuhusu uhamisho wa Wapalestina wanaoishi Gaza hadi katika eneo la nchi hizi za Kiafrika.
-
Onyo la Baraza la Wawakilishi la Yemen: Vikosi vya jeshi vitajibu ipasavyo
Baraza la Wawakilishi la Yemen limetoa taarifa likionya kuhusu matokeo ya hujuma za Marekani na Uingereza dhidi ya raia wa nchi hii.
-
Araqchi: Amerika haina haki ya kulazimisha (na kuelekeza) sera ya kigeni ya Iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Washington haina haki ya kulazimisha siasa za nje za Iran, na kuitaka kusimamisha mara moja mauaji yake kwa watu wa Yemen.
-
Ansarullah: Tutabaki na Gaza kwa gharama yoyote ile
Mjumbe Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah amesisitiza kuwa, Yemen haitaacha kuiunga mkono Palestina kwa gharama yoyote ile na akasema: Kila mtu anajua kuwa Yemen ni Mwaminifu katika kujibu hujuma ya adui, na Marekani inapaswa kusubiri jibu la Yemen.
-
Sheikh Rajab Shaaban:
Imam Hassan Al-Mujtaba (a.s) anazo fadhila nyingi na daraja ya juu
Tunayo mengi ya kujifunza kutoka ndani ya Qur’an Tukufu na kutoka kwa Itrah wa Mtume, Ahlul-Bayt wake Watoharifu (amani iwe juu yao), ambavyo ndio vizito vyetu viwili na viongozi wetu baada ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w). Na kumsoma na kumzungumzia Imam Hassan Al-Mujtaba (s.a), na kujifunza mengi kutoka kwake juu ya Uislamu wetu na Maisha yetu, ni sehemu ya kushikamana kisawa sawa na Ahlul-Bayt (a.s), ambao ndio kizito cha pili kwa ukubwa baada ya Qur’an Tukufu.
-
Sheikh Reihan Yasin:
Ramadhani ni Fursa ya Wakati
"Kila Muislamu anapaswa kuamini kuwa: Kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya wakati. Hivi ndivyo Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wa Mtume (a.s) pamoja na Masahaba wema walivyokuwa wakiamini, kwao Ramadhani haukuwa ni Mwezi kama Miezi mingine".
-
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dokta Abubakar Zuber Ali Mbwana:
"Maendeleo sio ugomvi, bali ni kufanya mambo yanayoonekana na yanayompendeza Mwenyezi Mungu"
Msikiti ni Nyumba ya Mwenyezi Mungu, na ni Kituo cha kiroho, kijamii na kiutamaduni, na vile vile ni nyumba makhsusi kwa ajili ya Waislamu kufanya ibada mbalimbali ndani yake.
-
UN: Hatua za kimataifa zichukuliwe dhidi ya ongezeko la 'chuki dhidi ya Waislamu'
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake juu ya "ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu", akitoa wito kwa serikali kulinda uhuru wa kidini, na kwa majukwaa ya mtandaoni kuzuia matamshi ya chuki.
-
Mustakbali uliogubikwa na kiza wa Syria; wafuasi wa al Julani wazidi kuua raia
Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria limeripoti habari ya kuuawa zaidi ya raia 1,383 wasio na hatia katika shambulio lililofanywa na magenge yenye mfungamano na watawala wa hivi sasa wa Syria kwenye maeneo ya Waislamu wa Kishia, magharibi mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Associated: Marekani na Israel zilitaka kuwapa makazi wakazi wa Gaza katika nchi tatu za Kiafrika
Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa Marekani na Israel zilitoa pendekezo kwa maafisa wa nchi tatu za Afrika la kuwapa makazi Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza kwenye ardhi za nchi hizo.
-
Waumini 80,000 wa Kipalestina washiriki Swala za Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa
Waumini wapatao 80,000 wa Kipalestina walishiriki swala ya Ijumaa ya pili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Msikiti wa Al-Aqsa jijini Al Quds (Jerusalem) licha ya vizuizi vikali vilivyowekwa na Israel kuwazuia Waislamu kufika katika eneo hilo takatifu.
-
Hamas yalaani marufuku ya pamoja ya US na EU dhidi ya al Aqsa TV
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani uamuzi uliochukuliwa na Marekani na Umoja wa Ulaya wa kupiga marufuku matangazo ya televisheni ya al Aqsa.
-
China na Russia zahimiza kuhitimishwa 'vikwazo haramu' dhidi ya Iran
Wanadiplomasia wa China na Russia wametoa wito wa kuondolewa "vikwazo visivyo halali" dhidi ya Iran, wakisisitiza kuwa Tehran inayo haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani.
-
Taifa la Iran halitalegeza kamba mbele ya vitisho vya mabeberu
Imamu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: "Taifa la Iran limethibitisha kuwa litasimama kidete kukabiliana na ubeberu na vitisho vya viongozi wa Marekani na halitalegeza kamba katika kutetea heshima na misimamo yake."
-
"Chuki dhidi ya Uislamu ni chombo cha kuhalalisha jinai za Israel"
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani mwenendo unaoongezeka wa kueneza chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu duniani na kusema kuwa, chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) ni nyenzo ya kuhalalisha uvamizi na jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Iran: Vikwazo vipya vimefichua unafiki wa Washington
Iran imelaani vikali vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu, Mohsen Paknejad na baadhi ya taasisi na meli zinazohusika na mauzo ya nje ya mafuta ya nchi hii na kusisitiza kuwa, vikwazo hivyo ni ithibati ya "ukiukaji wa sheria na unafiki" wa Washington.
-
Utawala wa Trump kuwapiga marufuku au kuwawekea mpaka wa kuingia Marekani raia wa nchi 43
Gazeti la New York Times limeandika katika toleo lake la leo kuwa serikali ya Donald Trump inapitia mpango wa kuwapiga marufuku au kuwawekea mpaka wa kuingia Marekani raia wa nchi 43.
-
Msemaji wa Serikali ya Iran: Uuzaji nje mafuta hauwezi kusitishwa
Msemaji wa Serikali ya Iran amesisitiza kuwa uuzaji nje mafuta wa Iran hauwezi kusimamishwa na hakukuwa na haja ya kuwekwa vikwazo vipya iwapo vile vya huko nyuma vilikuwa na taathira.
-
Uwepo wa magaidi kutoka nchi 20 katika Serikali ya Syria | Serikali ya mpito au Mradi wa Kikoloni!
Vyanzo vyenye maarifa na utambuzi, vimetoa taarifa juu ya kuundwa kwa muundo mpya wa usalama katika utawala wa Kigaidi wa al-Jolani.
-
Habari Pichani | Hamas: Kusimamisha idhaa ya al-Aqsa ni jaribio la kudhibiti sauti ya Wapalestina
Mtandao wa satelaiti wa Al-Aqsa umetangaza: Matangazo ya Idhaa ya Al-Aqsa yamesimamishwa katika Satelaiti zote za Kimataifa. Na Shirika lolote la Satelaiti litakaloendelea na urushaji wa matangazo na habari za Idhaa ya Al-Aqsa litakumbana na vikwazo vikubwa vya kiuchumi.
-
Karamu ya Iftar kwa watu 10,000 mahsusi kwa Mazuwwari wa Haram ya Imam Ridha (a.s) katika ua wa Imam Hassan al-Mujtaba (a.s.)
Kutokana na juhudi za Kitengo cha Maeneo Matukufu ya Madhabahu (Haram) Tukufu ya Razavi na katika mkesha wa kuzaliwa Ahlu al-Bayt (AS), Madhabahu Tukufu ya Razavi inawakaribisha mahujaji 10,000 waliofunga katika uwanja wa Imam Hassan Mojtabi (AS).
-
Msikiti wa Qur'an wa kuvutia nchini Uzbekistan
Nchini Uzbekistan, Msikiti mzuri umeundwa (umejengwa) ukiwa na Aya Tukufu za Qur'an zilizochongwa vizuri kwenye kuta zake.
-
Nijukumu letu sote kuwapenda na kuwajali Mayatima
"Nijukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha anamkumbusha mwenzake juu ya kuwapenda na kuwajali Mayatima na kutatua changamoto zao mbalimbali na kuwatimizia mahitaji yao".