-
Kamanda Irani: Nchi za kanda zinaweza kujidhaminia usalama
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa maadui wanapaswa kubadili mtazamo wao kuhusu kanda hii na kusisitiza kuwa nchi za kanda zinaweza kuhakikisha usalama wao wenyewe.
-
Wacanada wenye hasira wamjibu kivitendo Donald Trump
sambamba na hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump, ya kuongeza mashinikizo kwa Ottawa nwa vitisho vyake vya kuiteka Canada na kuijumuisha kwenye majimbo ya Marekani, wananchi wenye hasira wa Canada nao wameamua kutokaa kimya na wameanza kwa nguvu kutekeleza vikwazo dhidi ya bidhaa za Marekani.
-
UN: Utawala wa Trump uache kuingilia uhuru wa mahakama
Ripoti Maalumu wa Umoja wa Mataifa amekosoa vikali hatua za hivi majuzi za serikali ya Donald Trump ya kuwatimua na kuwateua maafisa wapya wa mahakama, akielezea wasiwasi wake kwamba hatua hizi ni sehemu ya vitisho kwa uhuru wa mfumo wa mahakama wa Marekani.
-
Wainjilisti wamshinikiza Trump kulipa wema, wamtaka aruhusu kunyakuliwa Ukingo wa Magharibi
Ripoti iliyochapishwa katika gazeti la Marekani, The New York Times, imefichua kwamba Wakristo wa Kiinjilisti, ambao walitoa huduma kubwa kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, wakati wa uchaguzi uliopita, ambapo karibu asilimia 80 walimpigia kura, sasa wanasubiri alipe fadhila na kuiruhusu Israel kutwaa Ukingo wa Magharibi, kwa madai ya ahadi ambayo eti Mungu aliwaahidi Wayahudi katika Biblia.
-
The Guardian: Trump anajifanya tu mbabe lakini ni mtu dhaifu
Gazerti la The Guardian la nchini Uingereza limeandika makala maalumu kuhusu misimamo dhaifu ya rais wa Marekani, Donald Trump katika masuala tofauti na kusema kuwa, ijapokuwa rais huyo anajifanya mbabe, lakini ni mtu dhaifu na vitisho vyake havina maana.
-
Mkutano wa Jeddah; licha ya kukamilisha lakini ni zaidi ya mkutano wa Cairo
Kufanyika mkutano wa dharura wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kiislamu huko Jeddah mara baada ya mkutano wa dharura wa mawaziri wa Mambo ya Nje na Wakuu wa Nchi za Kiarabu huko Cairo, Misri kunaonyesha ushirikiano wa pamoja wa Ulimwengu wa Kiislamu katika kukabiliana na mpango wa kuwafukuza kwa nguvu wakazi wa Ukanda wa Gaza na wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Yemen yatishia kuifungia tena Israel Bahari Nyekundu
Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen limeonya kuwa litarejea kwenye operesheni zake za kijeshi za majini za kuifungia Israel Bahari Nyekundu (Bahari ya Sham) kama Tel Aviv itashindwa kuheshimu muda iliopewa wa kukomesha mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
-
Indhari ya UN ya kutokea maafa ya kibinadamu Ukingo wa Magharibi kutokana na hujuma za Jeshi la Israel
Kufuatia kuendelea hujuma za jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu imetoa indhari kupitia taarifa yake kwamba uvamizi na hujuma za jeshi hilo katika eneo la kaskazini la Ukingo wa Magharibi zina madhara na maafa makubwa ya kibinadamu.
-
Mufti wa Oman asisitiza kuunga mkono Wapalestina wanaodhulumiwa Gaza
Mufti Mkuu wa Oman amewataka Waislamu wote na watu wanaopenda uhuru duniani kusaidia watu wanaodhulumiwa wa Gaza wanaoishi katika hali mbaya.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran inakataa kabisa sisitizo la kufanya mazungumzo na madola ya kibabe
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyid Ali Khamenei, amesema kuwa sisitizo la baadhi ya madola ya kibabe juu ya kufanyika mazungumzo na Iran halilengi kutatua matatizo.
-
Siku ya Wanawake; Iran yataka Israel itimuliwe UN
Ofisi ya Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa imetaka utawala wa Kizayuni utimuliwe kutoka kwenye umoja huo kutokana na jinai kubwa unazofanya dhidi ya wananchi wa kawaida wa Palestina hasa wanawake na watoto wadogo.
-
Iran: Machafuko nchini Syria ni kwa manufaa ya Israel
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, machafuko na ukosefu wa utulivu nchini Syria ni kwa manufaa ya utawala wa Kizayuni na kwamba magenge ya kigaidi na yenye misimamo mikali yanatumia vibaya fursa hiyo kwa manufaa yao binafsi.
-
Mkuu wa AEOI: IAEA iache kufanya mambo kisiasa kuhusiana na kadhia ya nyuklia ya Iran
Mohammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran AEOI, ameushauri Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA uache kutumia utashi wa kisiasa katika kadhia ya nyuklia la Iran.
-
Korea Kaskazini: Tutatoa jibu kali kwa maneva ya kijeshi ya Korea Kusini na Marekani
Korea Kaskazini imeionya Seoul na kutishia kuchukua hatua kali iwapo mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya kila mwaka kati ya Korea Kusini na Marekani yataendelea katika wiki zijazo.
-
Qalibaf: Iran haitasubiri barua yoyote kutoka Marekani
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema Jamhuri ya Kiislamu haisubiri barua yoyote kutoka kwa Marekani, kwani taifa hili linategemea uwezo wa ndani katika kukabiliana na changamoto zake.
-
Trump na kukandamizwa uhuru wa kusema huko Marekani
Gazeti la Marekani la Washington Post limeandika makala likiashiria amri za utendaji zilizotolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump, tangu aingie madarakani na kusema: Wakosoaji wanamtuhumu kuwa anakandamiza sana uhuru wa kujieleza na kukiuka Katiba ya Marekani.
-
Russia: Israel haina haki ya kuzungumzia miradi ya nyuklia ya Iran
Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Mashirika ya Kimataifa mjini Vienna, Mikhail Ulyanov, amesema kuwa utawala wa Israel hauna haki ya kutoa maoni kuhusiana na mpango wa amani wa nyuklia wa Iran.
-
China yaituhumu Marekani kuwa na sera za nyuso mbili
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imeutuhumu utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kufuata sera za " nyuso mbili" na kuahidi "kukabiliana kwa uthabiti" na mashinikizo yanayoongezeka ya vikwazo, huku mvutano kati ya nchi hizo mbili zenye nguvu za kiuchumi ukiendelea kutokota.
-
"Kutokomeza umaskini miongoni mwa wanawake kutachukua miaka 130"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameashiria matatizo yanayoendelea kuwakabili wanawake na wasichana duniani kote, akionya kwamba "kutokomeza umaskini uliokithiri miongoni mwa wanawake na wasichana kutachukua miaka 130."
-
Wacanada wenye hasira wamjibu kivitendo Donald Trump
sambamba na hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump, ya kuongeza mashinikizo kwa Ottawa nwa vitisho vyake vya kuiteka Canada na kuijumuisha kwenye majimbo ya Marekani, wananchi wenye hasira wa Canada nao wameamua kutokaa kimya na wameanza kwa nguvu kutekeleza vikwazo dhidi ya bidhaa za Marekani.
-
Nini kinaendelea Syria? Taasisi za kimataifa kimya!
Ukimya wa taasisi za kimataifa kuhusiana na mauaji ya umati dhidi ya raia nchini Syria yanayofanywa na viongozi wenye mafungamano na utawala wa al-Julani kwa mara nyingine tena unathibitisha undumilakuwili wa taasisi hizo.
-
OIC yalaani njama za kuhamishwa kwa nguvu Wapalestina Ghaza
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa taarifa rasmi mwishoni mwa kikao chake cha mjini Saudi Arabia na kulaani kwa nguvu zote njama za Marekani na Israel za kutaka kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
-
Sasa Trump ameelewa, HAMAS haimuogopi
Mchambuzi mmoja mashuhuri wa ulimwengu wa Kiarabu amesema: "Kulazimika Donald Trump kuomba kufanya mazungumzo ni matokeo ya kufeli na kukata tamaa serikali yake katika njama zake za kuilazimisha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS itii amri zake.
-
Kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake: Zaidi ya wanawake 12,000 wa Kipalestina wameuawa katika vita vya Gaza
Idara ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa: Wanawake 12,316 wa Kipalestina wameuawa shahidi katika vita vya mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni Israel dhidi ya watu wa Gaza.
-
Araghchi: Kuundwa nchi moja ya kidemokrasia ndiyo suluhu ya kadhia ya Palestina
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesisitiza tena msimamo wa Tehran wa kupinga eti 'suluhisho la mataifa mawili' kuwa njia ya kupata haki za Wapalestina na kusisitiza kwamba, uungaji mkono usioyumba wa Iran kwa kadhia ya Palestina bado upo thabiti.
-
Shutuma na bwabwaja za uwongo za Wamagharibi dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran
Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Miradi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa malengo ya amani haiwezi kuangamizwa kwa shambulio la kijeshi. Araqchi ameeleza haya akijibu uropokaji na uwongo wa Wamagharibi dhidi ya miradi ya nyuklia ya nchi hii.
-
Iran: Hakuna mazungumzo na Marekani wakati kuna vitisho na vikwazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema Tehran haitashiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja kuhusu nyuklia na Marekani maadamu Washington inaendelea na vikwazo vya upande mmoja na vitisho.
-
Netanyahu awazidishia vizuizi Wapalestina vya kusali Ijumaa Msikiti wa Al-Aqsa mwezi wa Ramadhani
Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ameidhinisha vizuizi vikali vya kuwekewa Waislamu Wapalestina kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa kwa ajili ya Sala ya Ijumaa wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Jeshi la Israel launda kifaa cha AI cha kuwajasisi Wapalestina
Uchunguzi mpya umefichua kuwa, kitengo cha ujasusi wa kielektroniki cha jeshi la Israel cha 8200 kimetumia mkusanyiko mkubwa wa mawasiliano yaliyonaswa kutengeneza chombo cha kijasusi cha Akili Mnemba (AI) ambacho modeli yake inashabihiana na ChatGPT, kwa lengo la kuwachunguza na kuwafanyia ujasusi wananchi wa Palestina.
-
70 wauawa katika mapigano baina ya pande kinzani Syria
Zaidi ya watu 70 wameripotiwa kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa nchini Syria kutokana na mapigano makali kati ya wanamgambo wa kundi la kigaidi linalotawala la Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) na makundi ya Muqawama ya wananchi huko magharibi mwa nchi hiyo.