-
Msikiti wa Mosalla Tehran kupanuliwa kuwa msikiti mkubwa zaidi duniani
Eneo kubwa la Swala la Tehran maarufu kama Mosalla Imam Khomeini litapanuliwa na kuwa msikiti mkubwa zaidi duniani.
-
Iran yasambaratisha mtandao wa magaidi wakufurishaji na kunasa silaha nyingi
Katika operesheni kubwa ya kupambana na ugaidi, vikosi vya usalama vya Iran vimesambaratisha mtandao mkubwa wa magaidi wakufurishaji na kukamata silaha na mabomu kadhaa katika mkoa wa kusini-mashariki wa Sistan na Baluchestan.
-
Baqaei: Kuna haja ya kuchukuliwa hatua za haraka kukomesha uvunjaji sheria wa Israel nchini Syria
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka kukomesha uvunjaji sheria wa utawala haramu wa Israel nchini Syria
-
Rais wa Iran ataka kuimarishwa uhusiano wa mataifa ya Waislamu
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amesema kuimarisha maelewano na uhusiano miongoni mwa nchi za Kiislamu zikiwemo Iran na Malaysia ni miongoni mwa mambo ya lazima katika hali ya sasa ya kimataifa.
-
The Economist: Ukraine inahitaji muda wa karne kadhaa kuweza kulipa deni la fedha kwa Marekani
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na gazeti la The Economist linalochapishwa nchini Uingereza, ikiwa Ukraine itatia saini makubaliano na Marekani ya kulipa fidia ya dola bilioni 500, kwa kuzingatia kasi yake ya sasa ya ukuaji wa uchumi, itahitaji mamia ya miaka ili kuweza kulipa deni lake hilo.
-
EU: Hatuwezi kuficha wasiwasi tulionao kuhusu matukio yanayojiri Ufukwe wa Magharibi, Palestina
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema, umoja huo hauwezi kuficha wasiwasi ulionao kuhusu matukio yanayojiri katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kwamba mzozo wa Palestina na Israel hauna ufumbuzi mwingine isipokuwa suluhu ya kuundwa mataifa mawili.
-
Vipigo vya Hizbullah vimeitia Israel hasara ya shekeli bilioni 9
Afisa mmoja wa utawala wa Kizayuni wa Israel amefichua kuwa, hasara iliyopatikana vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vya kaskazini mwa ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel, kutokana na vipigo vya Hizbullah wakati wa vita vya hivi karibuni inakadiriwa kuwa ni karibu shekeli bilioni 9 sawa na dola 2,515,582,638.
-
Sayyid Hassan Nasrullah alivunja kiburi cha jeshi la Israel linalodai halishindwi
Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa: Sayyid Hassan Nasrullah amepata mafanikio makubwa na kuvunja kiburi na majigambo ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ambalo linadai eti halishindiki.
-
HAMAS: Kuwa na silaha ni haki ya kisheria ya Muqawama na kuachana nazo ni jambo lisilowezekana
Hazem Qassem, msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ameashiria matamshi yaliyonasibishwa na kiongozi mwandamizi wa harakati hiyo Musa Abu Marzouk na kusisitiza kwamba: "Hamas inaendelea kutumia silaha za Muqawama kama haki halali na ya kisheria na haitalegeza msimamo juu ya suala hilo".
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Sayyed Nasrullah ni kielelezo cha ushujaa na muqawama
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Meja Jenerali Aziz Nasirzadeh, amesema kuwa, Katibu Mkuu wa Hizbullah, Shahidi Sayyed Hassan Nasrullah, alionyesha kielelezo cha kuigwa cha ushujaa na imani katika njia ya muqawama ambayo aliifuata.
-
Araqchi: Silaha za nyuklia za Israel ni tishio na hatari kwa dunia
Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa jamii ya kimataifa inapasa kuushinikiza utawala wa Israel kujiunga na Mkataba Unaozuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) ili shughuli zake za nyuklia ziwe chini ya usimamizi na ukaguzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA).
-
Kuendelea kupiga kambi kwa nguvu na satua msafara wa Manowari za Jeshi la Wanamaji la Iran katika maji ya kimataifa
Admirali Shahram Irani, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa Msafara wa Manowari Nambari 5 za jeshi hilo umepiga kambi katika eneo la maji ya kimataifa.
-
"Ulaya ndiyo iliyopata hasara kubwa katika kamari ya Trump na Putin"
Wakati huu ambapo Saudi Arabia inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano baina ya marais wa Russia na Marekani, kila kitu kinathibitisha kwamba aliyepata hasara kubwa katika kamari hiyo ni nchi za Ulaya.
-
Spika Qalibaf: Namna Hizbullah ilivyoonyesha nguvu zake imedhihirika kuwa Muqawama hauondosheki
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema, kutokana na jinsi Hizbullah ilivyoonyesha nguvu na uwezo wake, imemdhihirikia wazi kila mtu kwamba maadui hawawezi kuuondoa Muqawama au kuuweka kando ya ulingo wa kisiasa na kiusalama wa Lebanon kutokana na uungaji mkono wa wananchi ilionao.
-
WHO yasisitiza kuhusu makubaliano ya kuzuia majanga
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameonya kuwa historia haitazisamehe nchi ikiwa zitashindwa kuingia katika makubaliano ya kuzuia kwa pamoja majanga ya siku zijazo.
-
Vatican: Hali ya kiafya ya Papa Francis ni mbaya kutokana na tatizo la kupumua
Vatican imetangaza kuwa hali ya kiafya ya kiongozi wa Kanisa Katoliki mwenye umri wa miaka 88 bado ni mbaya.
-
Hizbullah: Adui Mzayuni hawezi kuusambaratisha muqawama
Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema: Adui Mzayuni hawezi kuusambaratisha muqawama.
-
Iran kuwakilishwa na Spika wa Bunge, Waziri wa Mambo ya Nje katika mazishi ya Shahidi Nasrallah
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) Mohammad Baqer Qalibaf na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi leo wanaelekea Beirut kushiriki katika hafla ya mazishi ya kiongozi wa Hizbullah aliyeuawa shahidi, Sayyed Hassan Nasrallah, pamoja na mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah, Shahidi Sayyid Hashim Safieddine.
-
Waziri Mkuu wa Yemen: Hizbullah imempigisha magoti adui Mzayuni
Waziri Mkuu wa Serikali ya Mabadiliko na Ujenzi ya Yemen amesema kuwa Harakati ya Muqawama ya Lebanon, Hizbullah, imempigisha magoti adui Mzayuni.
-
Hamas yakadhibisha madai ya kuwauwa mateka wa Kizayuni
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amekadhibisha vikali madai ya uwongo ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba harakati hiyo imewauwa mateka wake kadhaa wa Israel.
-
Familia ya Bibas yakataa kuwaruhusu mawaziri wa serikali ya Netanyahu kuhudhuria mazishi yake
Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa familia ya Shiri Bibas imesema kiongozi yeyote wa serikali ya Benjamin Netanyahu hapaswi kuhudhuria mazishi ya wana wao watatu, ambao miili yao ilirejeshwa siku chache zilizopita huko Israel kutoka Ukanda wa Gaza.
-
Mwanamke Mlebanoni aliyekaidi marufuku ya kuinua picha ya Nasrullah kwenye Uwanja wa Ndege wa Beirut azungumza
Asmaa Bzeih mwanamke kijana Mlebanoni mwenye umri wa miaka 27 ambaye amekuwa nembo ya upinzani baada ya hivi karibuni kukabiliana na maafisa husika katika uwanja wa ndege wa Beirut amesema kuwa dunia inapasa kuungana na Muqawama.
-
Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi awasalia Mashahidi wa Hizbullah, bahari ya umati wa watu yaifunika Beirut
Sheikh Muhammad Yazbek, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongoza Sala ya Maiti ya kusalia miili ya Mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiyyuddin katika mazishi ya kihistoria yaliyofanyika leo katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
-
Pezeshkian: Mashahidi Nasrullah na Safiyuddin walibakia watiifu kwa viapo vyao hadi mwisho
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaenzi na kuwakumbuka kwa wema Mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiyuddin wakati huu ambapo shughuli ya mazishi ya nguzo hizo mbili kubwa za kambi ya Muqawama ikiendelea.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Muqawama wa kukabiliana na ughasibu, dhulma na uistikbari si wa kumalizika
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu na ujumbe maalumu kwa mnasaba wa kufanyika mazishi na maziko ya Mwanajihadi mkubwa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Shahidi Sayyid Hashim Safiyyuddin na kusisitiza kuwa: "adui ajue kwamba, Muqawama wa kukabiliana na ughasibu, dhulma na uistikbari si wa kumalizika; na kwa idhini ya Allah utaendelea hadi ufikie lengo ulilokusudia".
-
Wafanyakazi wa EU walalamikia Brussels kuiunga mkono Israel
Makumi ya wafanyakazi wa Umoja wa Ulaya wamekusanyika Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji, kulalamikia uungaji mkono wa jumuiya hiyo kwa utawala wa Israel.
-
Ujerumani yajitutumua, yatoa onyo dhidi ya Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema Ulaya haipaswi kusita kuweka mashinikizo dhidi ya Marekani, iwapo Washington itashindwa kukumbatia 'demokrasia ya kiliberali'.
-
Israel yampiga marufuku msomi maarufu wa Kiislamu kuingia Msikiti wa Al-Aqsa
Vikosi vya utawala vamizi wa Israel vimemkamata na kumpiga marufuku Sheikh Najeh Bakirat, kiongozi mashuhuri wa Kiislamu Palestina kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa ulioko jijini Al Quds (Jerusalem).
-
HAMAS: Mateka 6 Waisrael wataachiwa leo mkabala wa Wapalestina 602 walioko kwenye jela za Israel
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza majina sita ya mateka Waisrael, ambao wanatazamiwa kuachiliwa leo katika mwendelezo wa awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kubadilishana mateka na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Madai yasiyo na msingi ya Trump na sisitizo lake la kuendeleza sera ya mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran
Akirejelea siasa zake za mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Donald Trump wa Marekani kwa mara nyingine tena amedai kuwa, siasa hizo zinalenga kuleta amani na kwamba Washington haitairuhusu Iran na nchi nyingine kupata silaha za nyuklia.