NYT yaagiza waandishi wake: Msitumie misamiati ya 'mauaji ya kimbari', 'uangamizaji wa kizazi' katika vita vya Israel
Taasisi ya uchunguzi wa taarifa za mitandaoni nchini Marekani ya Intercept imefichua kuwa gazeti la New York Times limewaagiza waandishi na maripota wake wa habari wanaoripoti vita vya mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza, wajizuie kutumia misamiati ya "mauaji ya kimbari" na "uangamizaji wa kizazi" na kupeuka kutumia neno “eneo linalokaliwa kwa mabavu” kumaanisha ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.