Mufti Mkuu wa Russia: Kiongozi Muadhamu wa Iran anastahiki kupongezwa
Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Waislamu ya Russia amesema kuwa, mwito unaotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei wa kuwataka watu wote duniani kuthamini masuala ya kidini na kimaadili unastahiki kupongezwa.