Trump atishia kuzikatia misaada Misri na Jordan na kutaka makubaliano ya kusitisha vita Ghaza yafutwe
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaweza akafikiria kusitisha msaada kwa Jordan na Misri ikiwa zitakataa kuwapokea Wapalestina, baada ya kutekeleza mpango wake wa kuwahamaisha kwa nguvu wananchi hao katika ardhi yao ya Ukanda wa Ghaza ili kulihodhi na kulimiliki eneo hilo lililowekewa mzingiro.