Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya amesema kuwa, kitendo cha Ufaransa cha kumuunga mkono jenerali Khalifa Haftari kiongozi wa wanamgambo wanaojiita Jeshi la Taifa la Libya ni cha aibu na fedheha.
Endelea ...-
-
Kumbukumbu ya mauaji ya Waislamu huko, Zaria kaskazini mwa Nigeria
Desemba 12, 2020 - 4:30 alasiriLeo Waislamu wa Nigeria wanakumbuka mauaji yaliyotekelezwa na jeshi la nchi hiyo katika mji wa Zaria jimboni Kaduna, dhidi ya wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
Endelea ... -
Wapalestina walaani hatua ya Morocco kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel
Desemba 11, 2020 - 7:32 alasiriHarakati za kupigania ukombozi wa Palestina zimelaani vikali hatua ya Morocco kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Endelea ... -
Nchi masikini kukosa chanjo ya COVID-19 baada ya nchi tajiri kuinyakua
Desemba 10, 2020 - 3:49 alasiriNchi tajiri duniani zimenunua kwa wingi chanjo ya COVID-19 au corona kwa ajili ya raia wao huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kuwa watu wa nchi masikini hawatapata chanjo hiyo muhimu.
Endelea ... -
Umoja wa Mataifa: Idadi ya wakimbizi duniani imepindukia milioni 80
Desemba 10, 2020 - 3:39 alasiriUmoja wa Mataifa umetangaza kuwa, idadi ya wakimbizi na watu waliolazimika kuhama makazi yao duniani imepindukia milioni 80 hadi kufikia katikati ya mwaka wa 2020.
Endelea ... -
Safari ya Rais wa Misri nchini Ufaransa na kupamba moto upinzani na malalamiko dhidi yake
Desemba 10, 2020 - 3:38 alasiriSafari ya hivi karibuni ya Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri nchini Ufaransa na mazungumzo aliyofanya na Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo vimeibua hasira na malalamiko ya waungaji mkono wa haki za binadamu.
Endelea ... -
UNICEF: COVID-19 imesitisha masomo ya mamilioni ya watoto
Desemba 10, 2020 - 3:37 alasiriShirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto, UNICEF limesema janga la COVID-19 au corona limepelekea mamilioni ya watoto ulimwenguni kusitisha masomo baada ya shule zao kufungwa.
Endelea ... -
Akufo-Addo achaguliwa kama rais wa Ghana kwa muhula wa pili
Desemba 10, 2020 - 3:32 alasiriNana Akufo-Addo amechaguliwa kwa muhula wa pili kuwa rais wa Ghana lakini mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo, John Mahama amepinga ushindi huo na kutangaza nia ya kuwasilisha malamiko mahakamani.
Endelea ... -
Katibu Mkuu wa UN awatolea mwito viongozi Kongo DR wamalize tofauti zao kwa njia ya mazungumzo
Desemba 10, 2020 - 3:31 alasiriKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani matukio ya ghasia yaliyofanyika katika siku mbili zilizopita ndani na nje ya jengo la bunge kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
Endelea ... -
Baraza jipya la mawaziri Tanzania laapishwa; Magufuli alitaka litekeleze majukumu yake
Desemba 10, 2020 - 3:29 alasiriRais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo amewaapisha mawaziri 21, na manaibu waziri 23 wa serikali yake mpya baada ya uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.
Endelea ... -
Rais wa Misri atupiwa lawama nyingine
Desemba 8, 2020 - 3:40 alasiriMashirika mengi ya haki za binadamu yamemtupia lawama chungu nzima Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri wakati huu wa ziara yake mjini Paris, Ufaransa.
Endelea ... -
Waziri wa Ulinzi wa Libya: Tutajitoa katika mapatano ya usitishaji vita iwapo Haftar atatekeleza shambulio la kijeshi
Desemba 8, 2020 - 3:37 alasiriWaziri wa Ulinzi wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya amesisitiza kuwa, hawana chaguo jingine ghairi ya kudhibiti maeneo yote ya nchi hiyo. Aidha ametishia kuwa, serikali yao itajitoa kwenye mapatano ya kusitisha vita iwapo kutajiri mashambulizi kutoka upande wa Jenerali Khalifa Haftar.
Endelea ... -
Taasisi za masuala ya kibinadamu zatahadharisha kuhusu maafa makubwa ya kibinadamu nchini Ethiopia
Desemba 8, 2020 - 3:36 alasiriTaasisi za masuala ya kibinadamu zimetahadharisha kuwa, eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia linakaribia kukumbwa na maafa ya kibinadamu na kuenea maambukizi ya kirusi cha corona kutokana na machafuko na ukosefu wa amani unaoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.
Endelea ... -
Ghasia zazidi kugubika kampeni za uchaguzi Uganda; wapinzani walalamikia rafu
Desemba 7, 2020 - 6:32 alasiriGhasia zinaendelea kuripotiwa katika kampeni za uchaguzi nchini Uganda ukiwa umebakia mwezi mmoja na wiki moja kabla ya kufanyika uchaguzi wenyewe hapo mwakani huku wapinzani wakilalamikia kile wanachokitaja kuwa kuandamwa na vyombo vya usalama.
Endelea ... -
Waziri: Jeshi la Sudan linafanya juhudi za kupanua uhusiano na Israel bila kuifahamisha serikali
Desemba 7, 2020 - 6:31 alasiriWaziri wa Habari wa Sudan ametangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo linafanya juhudi za kupanua uhusiano na utawala haramu wa Israel bila kuifahamisha serikali.
Endelea ... -
DRC: Mzozo wa vyama vya Kabila na Rais Tshisekedi wachukua sura mpya
Desemba 5, 2020 - 1:32 alasiriMvutano kati ya muungano wa vyama vinavyomuunga mkono Joseph Kabila (FCC) na muungano wa vyama vinavyomuunga mkono Rais Félix Tshisekedi huko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeshadidi na kuchukua sura mpya.
Endelea ... -
Polisi ya Uganda yajuta na kuomba msamaha baada ya mauaji dhidi ya wafuasi wa upinzani
Desemba 5, 2020 - 1:31 alasiriPolisi nchini Uganda imetangaza kuwa, inajuta kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji wa mgombea urais kupitia chama cha upinzani cha NUp cha Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine mwezi uliopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50.
Endelea ... -
Ripoti: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na baa kubwa la njaa
Desemba 5, 2020 - 1:30 alasiriShirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa, watu wapatao milioni 22 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanakabiliwa na ukosefu mkubwa chakula na hivyo kuhitajia misaada ya haraka ya chakula.
Endelea ... -
Marekani kuondoa wanajeshi wake Somalia kufikia Januari 2021
Desemba 5, 2020 - 1:28 alasiriMaafisa wa kijeshi wa Marekani wametangaza kuwa, majeshi ya nchi hiyo yaliyoko nchini Somalia muda si mrefu yataondoka katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika.
Endelea ... -
Jeshi la Ethiopia lateka na kuua akthari ya viongozi wa waasi wa Tigray
Desemba 5, 2020 - 1:27 alasiriSerikali ya Ethiopia imetangaza kuwa, imewakamata mateka na kuwaua akthari ya viongozi wa waasi wa Harakati ya Ukombozi wa Wananchi wa Tigray.
Endelea ... -
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria yalaani ugaidi wa Boko Haram
Desemba 5, 2020 - 1:15 alasiriOfisi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imelaani mauaji ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo yaliyofanywa na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram.
Endelea ... -
UN: Jangal la COVID-19 limesababisha ongezeko la watu masikini duniani kote
Desemba 4, 2020 - 10:42 alasiriRipoti mbili kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa zimeonesha namna athari za janga la COVID-19 lilivyosababisha kuporomoka kwa nguvu ya uchumi ya watu wengi duniani na hivyo kuwaingiza katika umaskini shadidi.
Endelea ... -
Makataa yaliyotolewa na Sudan kwa Marekani kwa ajili ya kupasisha sheria ya kuikinga dhidi ya mashtaka ya ugaidi
Desemba 3, 2020 - 3:47 alasiriLicha ya ahadi chungu nzima zilizotolewa na serikali ya Marekani kwa ajili ya kuondolewa Sudan katika orodha ya nchi zinazotuhumiwa kuunga mkono ugaidi na kuishawishi nchi hiyo ianzishe uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, lakini hakuna hatua yoyote ya maana iliyochukuliwa na serikali ya Washington katika uwanja huo, jambo ambalo limewakawasirisha viongozi wa Khartoum.
Endelea ... -
Mjumbe wa UN: Libya ina "hali mbaya sana" kwa kuendelea kuwepo wapiganaji 20,000 wa kigeni
Desemba 3, 2020 - 3:46 alasiriMjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ametahadharisha kuwa, kuwepo wapiganaji na mamluki wasiopungua 20,000 wa kigeni nchini humo kunaifanya "hali iwe mbaya sana" huku silaha zikiendelea kumiminika pia katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini iliyoharibiwa vibaya na vita.
Endelea ... -
Ofisi ya Sheikh Zakzaky: Boko Haram haliwakilishi Waislamu kwa namna yoyote ile
Desemba 3, 2020 - 3:45 alasiriOfisi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imelaani mauaji ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo yaliyofanywa na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram.
Endelea ... -
Algeria yautaka Umoja wa Afrika kutekeleze majukumu yake kuhusu Sahara Magharibi
Desemba 3, 2020 - 3:32 alasiriWaziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amesema kuwa Algiers inasikitishwa mno na hali ya Sahara Magharibi hususan matukio yaliyoshuhudiwa hivi karibuni na ameutaka Umoja wa Afrika AU utekeleze ipasavyo majukumu yake katika eneo hilo.
Endelea ... -
Rais wa Ghana atangaza mapumziko rasmi siku ya uchaguzi mkuu nchini humo
Desemba 3, 2020 - 3:31 alasiriRais wa Ghana, ameitangaza tarehe 7 mwezi huu wa Disemba kuwa ni siku ya mapumziko nchini humo ili kurahisisha zoezi la uchaguzi mkuu na kuruhusu ufanyike katika mazingira bora kabisa.
Endelea ... -
Umoja wa Mataifa wapasisha matumizi ya bangi kwa ajili ya matibabu
Desemba 3, 2020 - 3:22 alasiriTume ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na kudhibiti mihadarati imepiga kura na kupasisha matumizi ya bangi kwa ajili ya matibabu.
Endelea ... -
Kikao kijacho UN ni cha kadhia ya nyuklia ya Iran, A/Kusini ndiye mwenyekiti
Desemba 2, 2020 - 3:55 alasiriBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kuitisha kikao maalumu cha kujadili makubaliano ya nyuklia ya Iran mwishoni mwa mwezi huu wa Disemba.
Endelea ... -
Bobi Wine asitisha kampeni zake za urais baada ya kushambuliwa na polisi
Desemba 2, 2020 - 3:46 alasiriMgombea wa urais nchini Uganda kwa tiketi ya chama cha upinbzani cha NUP Robert Kyagulanyi, anayefahamika zaidi kama Bobi Wine, amesitisha kampeni zake, kufuatia kujeruhiwa kwa maafisa wake wa kampeni na kuharibiwa kwa gari lake Jumanne ya jana.
Endelea ...