Wanajeshi wananen wa Misri wauwawa kusini mwa Cairo / Daesh wadai kuhusika na mauaji hayo

  • Habari NO : 752968
  • Rejea : ABNA
Brief

Asubuhi ya leo watu waliokuwa na silaha wamefanya mashambulizi katika wilaya ya Halwani kusini mwa mji mkuu wa Misri na kupelekea vifo vya wanajeshi wa jeshi la Polisi wanane wa nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wananjeshi wanane wa jeshi la Polisi wauwawa akiwemo mmoja wao afisa wa usalam alfajiri ya siku ya jumapili kufuatia mashambulizi ya risasi yaliofanywa na watu waliokuwa na silaha pembezoni mwa wilaya ya Halawani kusini mwa mji wa Cairo.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa majeshi ya ulinzi wa nchi hiyo walifunga barabara ili kuzuia washambuliaji hao wasikimbie hatimaye kuwakamata lakini bila mafanikio.
Watu 4 waliokuwa na silaha ambao walikuwa wamepanda gari ndogo ya wazi baada ya kufungwa barabara hiyo, waliishambulia gari iliokuwa imebeba askali Polisi iliokuwa imepaki katika barabara hiyo.
Shirika la habari la Reuters limetangaza kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika kauli yake kuhusu tukio hilo, kauli amayo imesambazwa katika mitandao mbalimbali, lemekiri kuhusika na tukio hilo, ambapo walioshuhudia tukio hilo la kigaidi wamesema kuwa magaidi hao waliangusha bendera ya Daesh walipokuwa wanakimbia.
Kuuliwa kwa watu wanane wa jeshi la Polisi kwa siku mmoja na wakati mmoja katika tukio la kigaidi nchini Misri kumezusha gumzo kubwa katika vyombo vya habari, jamii na mitandao ya kijamii nchini Misri.
mwisho wa Habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Mourining of Imam Hossein
پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky