Wanajeshi 12 wa Misri wauwawa katika shamulio la kigaidi la Daesh

  • Habari NO : 794259
  • Rejea : ABNA
Brief

Wanajeshi 12 wa Misri wauwawa katika shambulio la kigaidi liliofanywa na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika sehemu ya kaskazini mwa jangwa la Sinai nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wanajeshi hao wameuwawa katika shambulio la kigaidi liliofanywa na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika kituo cha kijeshi cha ukaguzi cha jeshi la Misri katika eneo la kaskazini mwa jangwa la Sinai.
Katika shambulio hili magaidi hao walitumia gari liliotegwa bomu katika kufanya shambulio hilo, jambo ambalo limesababisa maafa makubwa ya wanajeshi wa jeshi la Misri, ambapo yawezekana idadi ya vifo ikazidi idadi iliotajwa.
  Mpaka sasa hakijatangaza rasmi kikundi gani kilichohusika na tukio hilo, ama kinachofahamika ni kwamba kikundi cha kigaidi cha Daesh ndio kilicho tangaza kupambana na majeshi ya Misri katika sehemu hiyo, asilimia kubwa inaonyesha kuwa kikundi hicho cha kigaidi ndio kilishohusika na tukio hilo.
Miaka ya hivi karibuni mashambulizi ya kigaidi yalishadidi katika jangwa la Sinai, ambapo mpaka sasa imeripotiwa kuuwawa mamia ya wanajeshi wa Misri kufuataia mashamulizi ya magaidi hao.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh kiliwataka wanachama wake wanao kiunga mkono kikundi hicho popote pale walipo, endapo watashindwa kwenda nchini Iraq na Syria wanaweza kwenda katika nchi ya Misri na Libya kwaajili ya kuungana na magaidi wa huko na kufanya mashambulizi ya kigaidi.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky