Mwimba Rap wa Daesh aangamia katika mji wa Musol

  • Habari NO : 796505
  • Rejea : ABNA
Brief

“Marwan Alwairi” mwemba rap maarufu kutoka Tunisia ambaye alijiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh ameangamia nchini Iraq kufuatia mashambulizi ya majeshi ya nchi hiyo katika makazi ya magaidi wa Daesh katika mji wa Musol

shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vyatangaza kuangamia kwa mwimba Rap maarufu wa Tunis aliyekuwa amejiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Musol nchini Iraq.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iraq “Marwan Alwairi” ambaye alijiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh, ameangamia kufuatia shambulio la wapiganaji wa majeshi ya Iraq dhidi ya magaidi hao katika mji wa Musol.
Aidha mwana mziki huyo alizaliwa mwaka 1990 nchini Tunisia, ambapo mnamo mwaka 2012 akiwa na miaka 22 alihukumiwa kifungo kwa kosa la madawa ya kulevya.
Baada ya kutoka kwake jela, kutokana na kuelemea kwake kwa fikra za vikundi vya kigaidi, kufuatia kushadidi kwa hali hiyo kwa vijana wa Tunis, serikali ya Tunis ilimkamata mwanamuziki huyo na kwa mara nyingine tena kuhukumiwa kifungo nchini humo kwa kosa la kujihusisha na mambo ya kigaidi.
Mwana muziki huyo wa kigaidi alijiunga na kikundi cha kigadi cha Daesh Baada ya kutoka kwake jela mwaka 2014 ambapo alisafiri kwenda Syria hatimaye kujiunga na kikundi hicho nchini humo.
Aidha baada ya kujiunga na kikundi cha kigaidi nchini Syria alianza kufanya kazi ya utangazaji katika redio ya kikundi cha kigaidi cha Daesh inayoitwa “albayan” iliopo katika mji wa Ar-Raqqeh nchini humo, ambapo baada ya muda uongozi wa kigaidi ulimwamisha na kumpeleka katika mji wa Musol, makao makuu ya kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq na huko ndiko alikoangamia gaidi huyo.


mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky