Sherehe kubwa za kuzaliwa Mtume (s.a.w.w) nchini Madagascar

  • Habari NO : 798518
  • Rejea : ABNA
Brief

Sherehe kubwa za kuzaliwa mtume Muhammad (s.a.w.w) zimepangwa kufanyika nchini Madagaska ambayo iatakuwa na anuani ya “sherehe za wafuasi wa Mustwafa (s.a.w.w)” ambapo itahudhuriwa na waislamu zaidi ya 700 wa nchi hiyo katika mji mkuu wa nchi hiyo (Antananarivo)

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wafuasi wa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) nchini Madagascar watafanya sherehe kubwa za kusherehekea kuzaliwa kwa mtukufu wa daraja Muhammad (s.a.w.w) chini ya anuani “sherehe za wafuasi wa Mustwafa (s.a.w.w)” ambayo itahudhuriwa na watu wengi miungoni mwa waislamu wa nchi hiyo.
Pia Sherehe hizo zitahudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali za Kiislamu nchini Madagascar, maimau wa sala za jamaa na Ijumaa, sherehe ambazo zitafanyika katika ukumbi mkubwa wa moja ya Hoteli kubwa ziliopo nchini humo.
Inasemakana kuwa wazungumzaji watakao zungumza katika sherehe hizo ni mmoja kati ya viongozi wa madhehebu za Kisunni, kiongozi mkuu wa jumuia ya Mahoja nchini humo, mwakilishi wa Jamiatul Al- Mustwafa (s.a.w.w) nchini humo na mmoja kati ya viongozi wa serikali ya Madagascar.
Sherehe hiyo iliokuwa na anuani ya “wafuas wa Mustwafa (s.a.w.w)” inafanyika kwa juhudi za chuo maalumu cha Al-Mustwafa nchini Madagascar kwa kuzishirikisha  taasisi saba za Kiislamu nchini humo.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky