Mashia wakusanyika mbele ya ikulu ya Marekani wakipeperusha bendera ya Imam Husein na kupinga ugaidi + Picha

  • Habari NO : 723501
  • Rejea : abna.ir
Brief

Waumini wa kiislamu wa dhehebu la Shia nchini Marekani wamekusanyika mbele ya ikulu ya Marekani White house na kupeperusha bendera ya Imam Husein a.s.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waumini wa kiislamu wa dhehebu la Shia  nchini Marekani wamekusanyika mbele ya ikulu ya Marekani White house na kupeperusha bendera ya Imam Husein a.s.

Mashia hao walikusanyika mbele ya ikulu kuomboleza na kuadhimisha arobaini ya Imam Husein a.s na kupinga matendo ya kigaidi yanayofanywa na makundi ya kigaidi na kuyanasibisha matendo hayo maovu na dini tukufu ya Uislamu ambayo ni dini iliyojengeka kwa misingi ya amani na utulivu.

Mashia ni dhehebu la kiislamu lenye kusifika kwa utulivu na misimamo inayokubalika kiakili, waislamu wa dhehebu la Shia kwa sasa wanaonekana kusikika kwa kasi kutokana na nafasi kubwa wanayoichukua katika kuhodhi siasa ya dunia, hii inatokana na athari kubwa za mapinduzi ya kiislamu ya Iran, ambayo ni Jamhuru ya kiislamu ya waislamu wa dhehebu la Shia.

Mashia wengi wanapatika katika nchi za Iraq, Iran, Yemen, Lebanon, Syria, Bahrain, India na hata Saudia arabia.

Wiki iliyopita ilikuwa ni siku ya kuadhimisha arobaini ya kifo cha mjukuu wa mtume Muhammad s.a.w ambaye aliuawa kikatili kwa kukatwa kichwa na Yazid bin Muawiyah.

Wiki iliyopita waislamu wa dhehebu la Shia zaidi ya milioni 27 walikusanyika katika mji wa Karbalaa Iraq wakiadhimisha arobaini ya tukio la Karbalaa, huu ni mkusanyiko mkubwa zaidi kushuhudiwa katika ulimwengu wa kiislamu, mkusanyiko huu unashinda hata ule wa Hijja ambapo kwa mwaka huu waislamu wapatao milion 2 na nusu walikwenda kuhiji Makkah.

Waislamu wa dhehebu la Shia wamecheza nafasi nzuri katika kupambana na ugaidi hasa katika nchi za Yemen, Syria na Iraq.

Mashia wamekuwa wakiuawa na waislamu wa dhehebu la Answari Sunna au mawahabi ambao wengi wao wanapatikana Saudia arabia, Pakistan, Misri, na Afghanistan.

Waislamu wa dhehebu la Answari sunna au wahabi wamekuwa wakiwazushia mashia kuwa ni makafiri na kuwashawishi waislamu maamuma wasio na elimu kuwa chukia mashia kuwa tenga na hata kuwaua.

Lakini kwa upande wa mashia wao hawana uadui na dhehebu lolote na wanapinga vikali kuhararisha kumwagwa damu za watu hovyo, kwani mtume Muhammad s.a.w hakuwa na silika hiyo.

mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni