Kumbukumbu ya miaka 70 ya mauaji ya wayahudi, yaliyopelekea kupatikana kwa nchi ya Israel

  • Habari NO : 684194
  • Rejea : abna.ir
Brief

Taifa la Israel ni taifa jipya lililopatikana kwa kudhulumu ardhi za waarabu kwa nguvu, katika dhuluma hiyo, Isrel ilipata msaada kutoka kwa Uingereza, Marekani na Ufaransa.
Jamhuri ya kiislam ya Iran, inasema kuwa inabidi ardhi zilizodhulumiwa zirudishwe kwa wahusika kwa thamani yeyote ile.

Leo dunia inakumbuka miaka 70 tangu kukombolewa kwa Mayahudi kutoka kambi za mauaji ya maangamizi dhidi ya jamii ya Kiyahudi barani Ulaya, yaliyopewa jina la Holocaust.

Ni mauaji haya yaliyopelekea baadaye kuundwa kwa taifa la Israel na hivyo kuigeuza kabisa historia ya ulimwengu kwa ujumla na hasa hasa ile ya Mashariki ya Kati.

Nchini Israel kwenyewe, watu walisimama kimya kwa muda wa dakika mbili, huku ving'ora vikilizwa nchi nzima kuwakumbuka wahanga wa mauaji hayo ya kikatili kabisa kuwahi kushuhudiwa duniani. Vituo vya redio na televisheni kote Israel vipindi na muziki wa maombolezo hayo.

Kumbukumbu hizi zilianza usiku wa Jumatano ambapo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aliitumia hotuba yake mbele ya maelfu ya watu waliokusanyika kwenye uwanja wa Makumbusho ya Yad Vashem mjini Jerusalem, kuyatupia lawama mataifa ya Magharibi, kwa kudharau khofu iliyonayo Israel dhidi ya uwezekano wa Iran kumiliki silaha za kinyuklia

"Makubaliano mabaya yanayoundwa pamoja na Iran yanaonesha kwamba dunia haikujifunza na tukio hili la kihistoria. Mataifa ya Magharibi yamepinda magoti mbele ya vitendo vya uchokozi vya Iran."

Mataifa sita makubwa duniani - Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Urusi, na China - yalifikia makubaliano na Iran juu ya programu hiyo mwezi uliopita. Baadhi ya mataifa hayo yalishuhudia mauaji makubwa ya Mayahudi wakati wa utawala wa Kinazi  wa Ujerumani miaka 70 iliyopita.

Netanyahu hana imani na makubaliano ya nyuklia ya Iran

Huku dunia nzima ikionekana kuungana kwenye kuunga mkono juhudi za kufikiwa suluhisho na Iran, Israel inajikuta ikiwa peke yake.  Hasa kutokana na misimamo mikali ya Iran dhidi ya uwepo wa  taifa la dhalimu la Israel ambalo baada ya wayahudi wengi kuuawa katika tukio la Holocaust, mayahudi walionusurika waliivamia nchi ya Palestina na kuwafukuza wakazi wa eneo hilo na kuanzisha nchi ya Israel.

Iran inataka Israel iondoke kwenye ardhi za Palestina ilizozinyakua kwa maguvu na kuwaacha wapalestina wakiwa huru.

Pamoja na Israel kupata msaada na utetezi mkubwa kutoka Uingereza, Ufaransa na Marekani bado inaonekana haiko katika amani kutokana na kuhofia hasira za waarabu iliyowazurumu ardhi zao kwa nguvu.

Mapema mwezi huu, Rais Barack Obama wa Marekani alionesha mara kadhaa kwenye hotuba yake kwamba Marekani inasimama bega kwa bega na Israel juu ya suala la usalama na kwamba hatoruhusu chochote kuuyumbisha usalama huo.

Hata hivyo, Netanyahu anaonekana kutoridhika na hakikisho hilo na ametumia pia hotuba yake ya leo kuifananisha Iran na utawala wa Ujerumani wa Kinazi katika kile kinachoonekana kuendeleza shinikizo lake dhidi ya makubaliano hayo ya nyuklia.

Waziri Mkuu huyo wa Israel Alisema:"Kama ambavyo Manazi walijaribu kuuharibu ustaarabu na kuwa na utawala wa "Kabila Kuu" huku wakiwafyeka Mayahudi, ndivyo Iran inavyojaribu kulitawala eneo hili na kutoka hapo kuendelea mbele zaidi kutekeleza lengo ililolitangaza la kulimwagia hewa ya sumu taifa la Mayahudi."

Iran imesema haiwezi kukaa kimya na kuona Israel ikiwaua raia wasiojiweza wa Palestina na Lebanon, na imeahidi kwamba taifa la Israel lazima liondolewe.

Wakati ambapo dunia inakumbuka miaka hiyo 70 ya mauaji ya Mayahudi wapatao milioni sita, utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tel Aviv nchini Israel unaonesha kuwa mashambulizi yanayohusishwa na chuki dhidi ya jamii hiyo yaliongezeka kwa asilimia 38 duniani mwaka 2014, ukiwa ni wa pili kuwa na mashambulizi kama hayo tangu mwaka 2009.

Kwa mujibu wa utafiti huo, mashambulizi au vitish vingi dhidi ya watu au taasisi za Kiyahudi yalitokea nchini Ufaransa ambako mwaka 2014 kulikuwa na matukio 164. Ufaransa ndio nchi ya Ulaya yenye idadi kubwa ya Mayahudi, ambao wanakisiwa kufikia 600,000.

Amiri jeshi mkuu wa Iran anasema kwamba taifa la Israel ni kiungo chenye kansa, hivyo kina takiwa kikatwe na kitakatwa.

Taifa la Israel ni taifa jipya lililopatikana kwa kudhulumu ardhi za waarabu kwa nguvu, katika dhuluma hiyo, Isrel ilipata msaada kutoka kwa Uingereza, Marekani na Ufaransa.

Jamhuri ya kiislam ya Iran, inasema kuwa inabidi ardhi zilizodhulumiwa zirudishwe kwa wahusika kwa thamani yeyote ile.


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky