Mfalme wa Saudi Arabia: mauaji ya mashia wa Nigeria ni katika kutokomeza ugaidi

  • Habari NO : 725666
  • Rejea : ABNA
Brief

Mfalme Salmani amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa jamhuri ya Nigeria (Muhammad Buariy) na kuyataja mauaji ya kikatili ya mamia ya mashia Wanigeria kuwa ni katika mpango wa kupambana na kutokomeza Ugaidi

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mfalme wa Saudi Arabia kwa mara ya kwanza baada ya kuuwawa kikatili mashia wa Nigeria na wanachama wa taasisi ya harakati ya Kiislamu kiongozi huyo amefanya mawasiliano hayo na Rais wa jamhuri ya Nigeria (Muhammad Buariy).
Katika mazungumzo hayo mfalme Salmani bin Abdilazizi alisema mauaji ya mamia ya mashia wa Nigeria ni moja kati ya njia za kupambana na kutokomeza ugaidi nchini humo, huku akisisitiza kuwa “uislamu umekemea harakati za waovu popotepale ulimwenguni nasi kama serikali ya Saudi Arabia  tutashirikiana kikamilifu na serikali ya Nigeria katika kukabiliana na kutokomeza ugaidi.
Naye amepinga hali ya mataifa ya kigeni kuingilia masuala ya ndani ya taifa la Nigeria na kusema: suala la nchi za nje kuingilia mambo ya ndani ya taifa la Nigeria ni kuisambaratisha hali ya utulivu na  amani iliopo ndani ya nchi hiyo, pia mfalme Salmani katika mazungumzo hayo alimshukuru Rais wa jamhuri ya Nigeria kwa kujiunga kwake katika jeshi la umoja wa nchi za Kiislamu ulioanzishwa na serikali yake hivi karibuni.   
mwisho wa Habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni