Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa asisitiza amani Syria

  • Habari NO : 739776
  • Rejea : abna.ir
Brief

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ameitaka serikali ya Syria na wapinzani nchini humo kuonyesha nia njema katika mazungumzo ya amani yanayotarajiwa kuanza kesho mjini Geneva

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ameitaka serikali ya Syria na wapinzani nchini humo kuonyesha nia njema katika mazungumzo ya amani yanayotarajiwa kuanza kesho mjini Geneva. Kauli hiyo ameitoa leo mjini Berlin, Ujerumani wakati wa mkutano wa pamoja na Kansela Angela Merkel. Akitoa maoni yake kuhusu mzozo wa wahamiaji barani Ulaya, Ban amesema ana wasiwasi kwamba baadhi ya nchi za Ulaya zinachukua hatua ambazo zinazuia harakati za wakimbizi kutafuta hifadhi. Amesema nchi hizo zinayakataa majukumu yao ya kibaadamu. Kwa upande wake Kansela Merkel amesema mapambano dhidi ya uhamiaji haramu ni sehemu ambayo wameiweka wazi na wanahitaji kufanya kila wawezalo kuhakikisha watu hawafi katika Bahari ya Aegean. Wakati huo huo, mtu mmoja ameuawa na mwingine amejeruhiwa baada ya kiasi ya makombora manane kurushwa kuelekea Uturuki kutoka kwenye mpaka wa Syria na kuushambulia mji wa Kilis.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni