Mahakama ya Uharifu yamtia hatiani makamu rais wa Congo

  • Habari NO : 742449
  • Rejea : abna.ir
Brief

Mahakama ya uhalifu ya kimataifa ya ICC imemkuta na hatia makamu wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Jean Pierre Bemba ...

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mahakama ya uhalifu ya kimataifa ya ICC imemkuta na hatia makamu wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Jean Pierre Bemba anaekabiliwa na mashitaka ya  kuwaamuru wanajeshi wake kufanya mauaji pamoja na vitendo vya ubakaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Hukumu hiyo ilitarajiwa kujikita zaidi juu ya wajibu wa kamanda kwa wanajeshi wake. Hii ni kesi ya kwanza  na ya aina yake katika mahakama hiyo ya ICC  inayohusiana na tuhuma za ukatili wa kingono zinazodaiwa kufanywa na wanajeshi katika maeneo ya migogoro. Akifanya majuuisho ya kesi hiyo mnamo mwaka 2014, mwanasheria wa upande wa mashitaka  Bala Gaye aliwaeleza majaji wa mahakama hiyo kuwa  wanajeshi wa Bemba walifanya vitendo vya ubakaji kila walipotaka kufanya hivyo. Hata hivyo wakili wa Bemba katika kesi hiyo alisema kulikuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Bemba kuhusiana na makosa hayo yakiwemo ya mauaji na ubakaji. 

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Mourining of Imam Hossein
پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky