Sheikh Zakizakiy anapaswa kuachwa huru ndani ya masaa 24 yajayo

  • Habari NO : 745805
  • Rejea : ABNA
Brief

Wakili mmoja wa Kinigeria ambaye aliruhusiwa kumuona na (Sheikh Zakizakiy) ameitaka serikali ya Nigeria kumwacha huru kiongozi huyo wa kikundi cha harakati ya Kiislamu ndani ya muda wa masaa 24 yajayo bila ya masharti yoyote.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wakili mmoja wa Nigeria ambaye alifanikiwa kuonana na kiongozi wa kikundi cha harakati ya Kiislamu nchini Nigeria (Sheikh Ibrahim Zakizakiy) katika jela za utawala wa Nigeria, baada ya kuonana naye ameitaka serikali ya Nigeria kumwacha huru kiongozi huyo bila ya masharti yeyote.
Kwa mujibu wa maelezo ya wakili huyo (Sheikh Zakizakiy na mke wake) kutokana na kupata majaraha makubwa wanahitaji kufanyiwa matibabu ya upasuaji, pia jicho la kushoto la Sheikh Zakizakiy limeathirika zaidi ambapo kama hali hiyo itazidi kuendelea yawezekana likashindwa kuona.
Tume ya Kiislamu ya haki za binadamu (IHRC) nayo imeunga mkono sauti ya wakili huyo na kuitaka serikali ya Nigeria haraka kumwacha huru kiongozi wa kikundi cha Harakati ya Kiislamu nchini humo.
Mwenyekiti wa tume hiyo amesema kuhusu suala hilo kuwa: serikali ya Nigeria daima imekuwa ikisisitiza kwa wananchi wake kufuata sheria ya jamhuri hiyo, hivyo kama bado inaendeleza kufuata kauli mbiu hiyo basi inapaswa haraka kumwacha huru Sheikh Zakizakiy na mashia wengine waliofungwa nchini humo, na wale wote walioshiriki katika jinai hizo wanapaswa kufunguliwa kesi katika mahakama za serikali ya Nigeria.
Kiongozi wa kikundi cha harakati ya Kiislamu nchini Nigeria na mke wake walikamatwa mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuvamiwa na majeshi ya nchi hiyo, na kuwapeleka sehemu isiofahamika.    
mwisho wa Habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni