Serikali ya Rwanda yawafukuza Warundi 1,500

  • Habari NO : 754704
  • Rejea : abna.ir
Brief

Maafisa wa Rwanda wamesema wamewafurusha kutoka nchini humo zaidi ya raia 1,500 wa Burundi katika siku za hivi karibuni

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Maafisa wa Rwanda wamesema wamewafurusha kutoka nchini humo zaidi ya raia 1,500 wa Burundi katika siku za hivi karibuni. Waziri wa kushughulikia mikasa na masuala ya wakimbizi wa Rwanda Seraphine Mukantabana amesema kufurushwa huko kwa raia wa Burundi ni sehemu ya msako wa kawaida wa wanaoishi kinyume na sheria nchini Rwanda na sio msako wa kuwalenga hususan Waburundi. Uhusiano kati ya nchi hizo jirani umekuwa ukizorota. Msako huo wa Rwanda unafuatia wa Burundi uliopelekea maelfu ya Wanyarwanda kufurushwa tangu mwezi Aprili mwaka jana. Burundi imekuwa katika mzozo wa kisiasa tangu mwaka jana baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombea muhula wa tatu madarakani na kuchochea maandamano na ghasia ambazo zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 500 na kusababisha wengine 250,000 kuyatoroka makaazi yao. Burundi inaishutumu Rwanda kwa kuwafadhili waasi wanaotaka kumng'oa madarakani Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imeyakanusha vikali.

Mwisho wa habari/ 291


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Mourining of Imam Hossein
پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky