Helikopta ya Urusi yadunguliwa na kuuwa watano + Picha

  • Habari NO : 769445
  • Rejea : abna.ir
Brief

Magaidi wanaoungwa mkono na Marekani ndio wahusika wakuu wa udunguaji huo.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Watu watano wameuwawa wakiwa ndani ya helikopta ya Urusi iliyodunguliwa juu ya anga ya Syria leo,  hilo likiwa ni tukio la maafa makubwa kutokea kwa wakati mmoja kwa Urusi tokea nchi hiyo iingilie kati katika vita vya Syria. Shambulio hilo linakuja wakati wapiganaji wa upinzani wa Syria na washirika wao kigaidi ambao wote wanadhaminiwa na Marekani wakipambana na vikosi vya serikali nje ya Aleppo katika jaribio la kutaka kupunguza makali ya mzingiro wa serikali dhidi ya vitongoji vinavyoshikiliwa na magaidi wanaounga mkono na Marekani katika mji huo ulioko kaskazini mwa Syria.Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa helikopta hiyo ya kijeshi ya kusafirisha mizigo iliokuwa na maafisa wawili na wafanyakazi watatu imedunguliwa kutoka ardhini baada ya kuwasilisha misaada ya kibinadamu huko Aleppo. Ikulu ya Urusi imesema watu wote waliokuwemo ndani inachukuliwa kuwa wamekufa na kwamba wamekufa kishujaa wakati walipokuwa wakijaribu kuepusha helikopta hiyo isisababishe maafa makubwa ardhini.

Magaidi wanaoungwa mkono na Marekani ndio wahusika wakuu wa udunguaji huo.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky