Saudia arabia yaua watu zaidi ya 700 Yemen + picha

  • Habari NO : 784501
  • Rejea : abna.ir
Brief

: katika kipindi ambacho Marekani na washirika wake wanaosaidia upande wa magaidi nchini Syria wameitisha kikao cha dharura umoja wa mataifa, ili kuishinikiza serikali ya Syria aiche mashambulizi ya anga dhidi ya magaidi katika mji wa Allepo, Majeshi ya Saudia arabia yamefanya mashambulizi dhidi ya raia na kupelekea kuawa zaidi wa raia wasio na hatia 150.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa:  katika kipindi ambacho Marekani na washirika wake wanaosaidia upande wa magaidi nchini Syria wameitisha kikao cha dharura umoja wa mataifa, ili kuishinikiza serikali ya Syria aiche mashambulizi ya anga dhidi ya magaidi katika mji wa Allepo, Majeshi ya Saudia arabia yamefanya mashambulizi dhidi ya raia na kupelekea kuawa zaidi wa raia wasio na hatia zaidi ya 700.

Maelfu ya Wayemen wamefanya maandamano katika mji mkuu Sanaa hii leo, wakilaani shambulizi la angani lililofanywa jana katika ukumbi wa ibada ambalo Umoja wa Mataifa umesema liliwaua watu 700 na kuwajeruhi zaidi ya 500. Maandamano hayo, yalioungwa mkono na wafuasi wengi wa wapiganaji wa Houthi wanaoipinga serikali ya kidhalimu ya Mansur hadi, yaliandaliwa karibu na ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Sanaa ambako waandamanaji hao walitoa kauli mbiu za kuupinga muungano wa kiarabu unaoua watu nchini Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia na kuungwa mkono na Marekani, uingereza, ufaransa na Israel ambapo wanaulaumu dhulma na mashambulizi yanayofanywa dhidi yao kwa zaidi ya mwaka sasa bila ya msaada wa Umoja wa mataifa.

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameitisha uchunguzi wa haraka na usioegemea upande wowote kuhusiana na shambulizi hilo. Saudia arabia imekataa kuhusika na Shambulizi hilo la ndege, Nayo Marekani  ambayo ndio mdhamini mkuu wa mashambulizi hayo imetangaza kuwa inatathmini upya msaada wake kwa muungano huo wa Kiarabu.

Iran imekuwa ikitoa malalamiko kwa Umoja wa mataifa kuitazama Yemen, na kutetea haki za wanyonge lakini umoja wa mataifa umeziba masikio na kulifumbia macho suala hilo kutokana na mashinikizo kutoka kwa Marekani na washirika wake.

Baada ya kufanya shambulizi hilo, majeshi ya Saudia arabia hayakutosheka bali yaliendelea  kushambulia na magari ya hospitali yaliyofika kutoa msaada eneo la tukio.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Mourining of Imam Hossein
پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky