Morocco baada ya miaka 8 yafungua ubalozi wake nchini Iran

  • Habari NO : 785721
  • Rejea : ABNA
Brief

Mfalme wa Morocco baada ya miaka 8 ya kukata uhusiano wa kidiplomasia na Iran ameamua kuainisha balozi wake mpya mjini Teheran

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Muhammad VI mfalme wa Morocco amemuanisha balozi wake mpya wa mjini Teheran, balozi ambaye ndiye balozi wa kwanza nchini Iran kutoka nchini Morocco baada ya kukata uhusiano wa Kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili mnamo mwaka 2009.
“Hasan Hami” ambaye ni balozi wa zamani wa Morocco katika jamhuri ya Azerbaijan, ndiye ameanishwa kuwa balozi mpya wa Morocco mjini Teheran.
Mnamo mwaka 2009 serikali ya Morocco ilisitisha fungamano lake la kidiplomasia na Iran, kwa madai kuwa Iran ina lengo la kueneza madhehebu ya Shia nchini humo, ambapo katika mwaka huohuo mwezi Machi serikali ya Morocco iliutuhumu ubalozi wa Iran mjini Rabat (mji mkuu wa Morocco) kuwa unafanya juhudi za kuisambaratisha serikali ya kifalme ya nchini hiyo, nakuleta hitilafu baina ya wafuasi wa madhehebu za nchi hiyo, ambapo Iran ilipinga tuhuma hizo.
Vyombo vya habari vya Morocco vimetangaza kuwa toka mwaka 2014 viongozi wa nchi hizo mbili walikuwa wakifanya mazungumzo ya mara kwa mara kwaajili ya kurudisha uhusiano wao, na katika mwaka huohuo fungamano la kidiplomasia la nchi hizo mbili lilirudi katika hali ya kawaida, ambapo Iran ilimtuma Muhammad Taqiy Muayid kuwa ni balozi wa Iran nchini Morocco, ambapo balozi wa Iran nchini Morocco alianza kazi zake rasmi mnamo mwezi Januari mwaka 2015 katika mji mkuu wa nchi hiyo Rabat.
mwisho wa Habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky