Uchaguzi wa rais Congo wapelekwa mbele hadi Aprili 2018

  • Habari NO : 785973
  • Rejea : abna.ir
Brief

: Vyama vinavyounda muungano unaotawala Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na vyama vyengine vidogo vimekubaliana kuchelewesha uchaguzi wa mwezi ujao hadi Aprili mwaka 2018 hatua itakayoyakasirisha makundi ya upinzani.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Vyama vinavyounda muungano unaotawala Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na vyama vyengine vidogo vimekubaliana kuchelewesha uchaguzi wa mwezi ujao hadi Aprili mwaka 2018 hatua itakayoyakasirisha makundi ya upinzani.

Kundi kuu la upinzani nchini Congo halikuweza kupatikana mara moja kuzungumzia uamuzi huo lakini tayari limeitisha mgomo wa taifa hapo Jumatano kumshinikiza Rais Joseph Kabila kuachia madaraka mwishoni mwa muhula wake hapo mwezi wa Disemba.

Kundi hilo kuu la upinzani linaloongozwa la Etiene Tshisekedi limesusia mazungumzo ya usluhishi wa kitaifa kwa hoja kwamba ni ni njama za Rais Kabila kuendelea kun'gan'gania madaraka.

Mwezi uliopita madazeni ya watu waliuwawa wakati wa maandamano ya siku mbili mjini Kinshasa kupinga mipango ya kuchelewesha uchaguzi huo kwa kile serikali inachosema matatizo ya kifedha na vifaa katika kuwaandikisha mamilioni ya watu katika nchi kikubwa ya kimaskini.

Muda zaidi kwa dafatri la wapiga kura

Vyama hivyo vimekubaliana hapo Jumamosi kutowa muda zaidi kwa daftari la kuandikisha wapiga kura na kumuachia Kabila endelee kubakia madarakani hadi uchaguzi huo uliocheleshwa utakapofanyika hayo ni kwa mujibu wa chama kimoja kilichohudhuria mazungumzo hayo Union for Congolese Nation (UNC).Wajumbe katika mazungumzo hayo yumkini wakaidhinisha uamuzi huo hapo Jumatatu.

Rais wa chama hicho cha UNC Vital Kamere anatarajiwa sana kuwa Waziri Mkuu kama sehemu ya serikali ya mseto inayopendekezwa chini ya mazungumzo hayo.

Kabila ambaye ameingia madarakani hapo mwaka 2001 kufuatia kuuwawa kwa baba yake amesema ataheshimu katiba lakini hakufuta uwezekano wa kujaribu kubadili sheria za nchi hiyo kumwezesha kuwania muhula mpya .

Hatari ya kukosa utulivu

Marais wa nchi jirani za Rwanda na Jamhuri ya Congo walibadili katiba zao mwaka jana ili kuwawezesha kuwania muhula wa tatu na wapinzani wa Kabila wanasema wana hofu Kabila naye atafanya hivyo hivyo.

Mamia ya watu pia wamekufa tokea mwaka jana katika nchi jirani ya Burundi baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kutaka kuwania muhula wa tatu madarakani na kusinda katika uchaguzi ambao wapinzani wake wamesema ulikuwa kinyume na katiba.

Mkuu wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Congo ameonya wiki iliopita kwamba mkwamo wa kisiasa unatowa tishio kubwa sana la kuifanya nchi hiyo kukosa utulivu.

Mamilioni ya watu wamekufa katika mizozo ya kanda kati ya mwaka 1996 na 2003 na Congo katu haikuwahi na tajiriba ya kukabidhiana madaraka kwa amani.

Mwisho wa habari/ 291

 

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky