Ufaransa yasitisha shughuli za kulinda amani Jamhuri ya Afrika Kati baada ya kufanya uhalifu mkubwa

  • Habari NO : 789048
  • Rejea : abna.ir
Brief

serikali ya Ufaransa imetangaza kulitoa jeshi lake lililokwenda kwa ajili ya kulinda amani Afrika ya kati, na badala yake wanajeshi hao walikuwa wakibaka wananchi na kupendelea upande wa magaidi wa kikristo waliokuwa wakuchinja na kuuwa waislamu nchini humo.

Shirka la habari la ABNA linaripoti kuwa: serikali ya Ufaransa imetangaza kulitoa jeshi lake lililokwenda kwa ajili ya kulinda amani Afrika ya kati, na badala yake wanajeshi hao walikuwa wakibaka wananchi na kupendelea upande wa magaidi wa kikristo waliokuwa wakuchinja na kuuwa waislamu nchini humo.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema nchi yake itakuwa tayari kuingilia kati katika jamhuri ya Afrika Kati, ikilazimika, licha ya kusitisha shughuli zake za kulinda amani katika koloni lake hilo la zamani. Ufaransa ilianzisha opereshini Sangaris decemba mwaka 2013 kujaribu kumaliza mauwaji yaliyoripuka ambapo kundi la magaidi wa kikristo laAnti Balaka lilikuwa likivamia na kuwaua kinyama wananchi wa kiislamu. Vikosi vya kulinda amani vya Ufaransa vilifikia watu 2000-lakini vinatazamiwa kupunguzwa hadi 300 hadi ifikapo mapema mwakani. Wengi wao watawekwa katika kituo cha mafunzo ya kijeshi kinachosimamiwa na Umoja wa ulaya pamoja na kusaidia opereshini za ndege zinazoruka bila ya rubani zinazoendeshwa na Umoja wa Mataifa,au kuvisaidia vikosi vya jeshi la serikali. Shughuli za usalama zitadhibitiwa na wanajeshi 13000 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa baada ya vikosi vya Ufaransa kuondoka. Hata hivyo vikosi hivyo vinazidi kukosolewa na raia kwamba havifanyi chochote kulinda usalama zaidi ya kubaka wananchi. Ufaransa haitaiacha Jamhuri ya Afrika Kati" amesema Le Drian mbele ya bunge mjini Bangui,alikofika kwa lengo la kutangaza kumalizika opereshini Sangaris.

Mwisho wa habari/ 291

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky