Serikali ya Kenya yapanga kuondoa askari wake nchini Sudan Kusini

  • Habari NO : 789640
  • Rejea : abna.ir
Brief

Siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kumfuta kazi kamanda wa Kenya Johnson Mogoa Kimani Ondieki aliyekuwa akikiongoza kikosi cha kulinda amani cha Umoja huo nchini Sudan Kusini,

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kumfuta kazi kamanda wa Kenya Johnson Mogoa Kimani Ondieki aliyekuwa akikiongoza kikosi cha kulinda amani cha Umoja huo nchini Sudan Kusini, Kenya imesema kwamba inaviondoa vikosi vyake kutoka katika ujumbe wa kulinda amani Sudan Kusini. Wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema katika taarifa yake kwamba kuendelea kupelekwa kwa askari wake nchini Sudan Kusini hakutawezekana na kwamba inajali ustawi na usalama wao. Taarifa hiyo imeongeza kwamba Kenya haitaendelea na mipango ya kuchangia askari wake katika kikosi cha ulinzi na inajitoa katika mchakato wa amani wa Sudan Kusini. Kenya ina jumla ya askari 1000 katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani katika taifa la Sudan Kusini na ilikuwa imeahidi nyongeza ya askari wengine 4000.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky