Kuwasili kwa makomandoo elfu 3 wa Misri nchini Syria

  • Habari NO : 789818
  • Rejea : ABNA
Brief

Kwa mara ya kwanza kwa serikali ya Misri, kutuma majeshi yake nchini Syria ili kuisaidia nchi hiyo katikia kupambana na vikundi vya kigaidi nchini humo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: baadhi ya vyombo vya habari vimeandika kuwa makumi ya wanajeshi wa Misri wameingia nchini Syria kwaajili ya kuungana na taifa hilo katika kupambana na vikundi vya kigaidi pia kupata mafunzo ya kukabiliana na magaidi kupitia majeshi ya Urusi, wanajeshi hao wamefikia katika bandari ya Tartus nchini Syria.
Tovuti ya Al Masdar New ikisambaza habari hii imesema kuwa: vyanzo makini vya sehemu husika inasema kuwa siku ya Alhamisi iliopita kiasi cha wanajeshi wa Misri wamejiunga na majeshi ya Urusi katika bandari ya Tartus nchini Syria.
Jeshi la Urusi nchini Syria lina kambi mbili za kijeshi ambapo moja kati ya mbili hizo ni lipo katika bandari ya Tartus nchini humo.
Aidha tovuti hiyo  imebainisha kuwa: hatua ya Misri ya kutuma jeshi katika kuisaidia Syria ni hatua ya kwanza ya serikali ya Cairo inayoashiria mwanzo wa kurudisha uhusiano baina ya mataifa hayo katika hali ya kawaida, hasa baada ya kusambaratika uhusiano wa serikali ya Misri na utawala wa kifalme wa Saudi Arabia, hususan katika kutafautiana mitazamo ya mataifa hayo kuhusu suala Syria.
Mmoja kati ya viongozi wa serikali ya Syria ametangaza habari ya kuingia makomandoo 3000 kutoka nchini Misri, ambapo majeshi ya Misri yatangaza kuwa, kuingia kwa wanajeshi hao ni kwaajili ya kuongeza nguvu kwa majeshi ya Syria katika kupambana na vikundi vya kigaidi hususan katika kuikomboa wilaya ya Halab nchini humo.
Aidha amesema kuwa: Jenerali Abdel Fattah el-Sisi “Rais wa jamhuri ya Misri” kwa maamuzi hayo ya kutuma majeshi yake kuungana na majeshi ya Syria katika kukabiliana na vikundi vya kigaidi, ni kuitambua haki ya serikali ya Syria na washirika wake.
Kutokana na maelezo ya chanzo hicho muhimu ni kwamba kutumwa kwa wanajeshi hao ni kiashirio cha kurejea kwa fungamano la nchi hizo katika hali ya kawaida, ambapo fungamano la nchi hizo liliingia dosari pale tu baada ya Rais aliyepita wa Misri (Muhammad Mursiy) kukataa kuwa na fungamano lolote na serikali ya Syria toka mwaka 2012.       
mwisho wa Habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky