Watu 10 katika waombolezaji za Arubaini ya Imam Husein wauliwa na majeshi ya Nigeria + picha

  • Habari NO : 791968
  • Rejea : ABNA
Brief

Washiriki wa maombolezo ya ishara ya arubaini ya Imam Husein (a.) mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika wilaya ya Kaduna nchini Nigeria washambuliwa na majeshi ya nchi hiyo na kusababisha vifo na kujeruhiwa waombolezaji hao.

Shirika la habari la Ufaransa limetangaza kuwa jeshi la polisi nchini Nigeria limeuwa watu takriban 10 katika maombolezo ya kuadhimisha siku ya arubaini ya Imam Husein nchini humo.
Walio shuhudia tukio hilo wamesema kuwa: jeshi la Polisi la Nigeria limeshambulia maombolezo hayo nje kidogo ya mji wa Kanu mashariki mwa nchi hiyo, huku mmoja kati ya walioshuhudia tukio hilo akisema kuliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa: kwa uchache miili ya watu iliokuwa imepigwa risasi na kuanguka chini ni zaidi ya 15, lakini vyombo vya habari vitangaza kuwa ni watu 10 tu.
Aidha aliongeza kusema kuwa Polisi wa  majeshi ya Nigeria yalichukua miili ya watu hao waliokuwa wamefariki na kuipeleka sehemu nyingine.
Polisi mmoja aliokuwa ameshiriki katika mauaji hayo, baada ya kuthibitisha kutokea kwa mauaji hayo amedai kuwa waandamanaji hao walikuwa wanafanya fujo na vurugu.
Kikundi cha harakati ya Kiislamu Nigeria kimetangaza kuwa wafuasi wa madhehebu ya Shia asubuhi ya Jumatatu walikuwa wamefanya maambulezo hayo ikiwa ni ishara ya siku ya arubaini ndipo majeshi ya Polisi ya Nigeria wakashambulia maadhimisho hayo.
Aidha katika ujumbe wa kikundi hicho cha harakati ya Kiislamu Nigeria: jeshi la Polisi la Nigeria walivamia maombolezo hayo ya suluhu na amani katika barabara kuu ya Kanu na kuwarushia risasi waombolezaji, hii ni katika mipango ya kishetani iliopangwa na serikali ya Nigeria.
Kwamujibu wa ripoti hii ni kwamba majeshi ya polisi nchini humo walitumia mabomu ya machozi na risasi za kivita dhidi ya waombolezaji hao.
Inasemakana kwamba.

    
mwisho wa Habari


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky