Umoja wa Ulaya waiwekea vikwazo serikali ya Syria kwa kosa la kupambana na magaidi

  • Habari NO : 791998
  • Rejea : abna.ir
Brief

Umoja wa Ulaya ambao umechanganyikiwa kufuatia ushindi wa Trump, Umeiwekea vikwazo serikaki ya Syria kwa kosa la kupambana na magaidi ambao Umoja huo na Marekani unawadhamini.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Umoja wa Ulaya ambao umechanganyikiwa kufuatia ushindi wa Trump, Umeiwekea vikwazo serikaki ya Syria kwa kosa la kupambana na magaidi ambao Umoja huo na Marekani unawadhamini.

Hatua hiyo ya haraka imekuja baada ya Ushindi wa Trump ambaye aliahidi kuacha kusaidia magaidi nchini Syria na badala yake kusaidiana na Urusi na Iran katika kupambana na magaidi hao, ambao Umoja wa Ulaya, Marekani na mataifa ya kiarabu yametumia pesa nyingi kuwaanda na kuwasaidia magaidi hao ili waiangushe serikali ya kidemokrasia ya Syria kama walivyofanya kwa serikali ya Muammar Gaddafi wa Syria.

Sanjari na hayo Umoja huo umewawekea vikwazo mawaziri 17 wa Syria na gavana wa benki kuu. Vikwazo hivyo vimewekwa kwa ajili ya kulenga kuidhoofisha serikali ya Rais Bashar al-Assad wa Syria, ambao umekuwa ukifanya mashambulizi dhidi ya magaidi wanaoungwa mkono na Umoja huo. Vikwazo hivyo ni pamoja na marufuku ya kusafiri na kutaifisha mali zao kama sehemu ya mkakati wake wa kuiangusha serikali ya Assad ambayo inaungwa mkono na Urusi na Iran. Taarifa ya Umoja wa Ulaya imeeleza kuwa uamuazi huo umeongeza orodha ya watu waliowekewa vikwazo na kufikia 234. Taasisi nyingine 69 zinalengwa kuwekewa vikwazo vya kutaifishiwa mali zao.

Umoja wa Ulaya umeweka vikwazo hivyo baada ya magaidi wanaowaunga mkono kuelemewa kwenye uwanja wa vita, pia umoja huo umepata hofu kubwa baada ya Trump kuchaguliwa kuwa rais, ambapo aliahidi kuacha kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika njama ovu za kuiangusha serikali ya Syria. Hivyo umoja huo unataka kutumia muda wa mwisho wa utawala wa Obama kuiangamiza serikali ya Syria.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky