Shule na Huseinia yabomolewa na serikali ya Nigeria + picha

  • Habari NO : 793184
  • Rejea : ABNA
Brief

Shule ya Kiislamu ya Fidyah iliopo katika wilaya ya Zaria na Huseinia ya mashia katika sehemu ya Saminaka nchini Nigeria yabolewa na majeshi ya Serikali ya Kaduna nchini humo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari za kubolewa kwa Huseinia ya mashia wa mji wa Zaria katika wilaya ya Kaduna zasambaa ambapo amri hiyo imetolea na serikali ya jimbo hilo.
Aidha ripoti za kubomolewa kwa shule ya kiislamu katika wila hiyo zimetufikia, ambapo kituo cha mafunzo kiliokuwa na jina la (kituo cha elimu ya msingi na sekondari) katika jimbo la Kaduna, shule ambayo ilikamilisha njia zote za usajili mpaka kukamilika kwake.
Kwa mujibu wa ripoti hii, shule ya Kiislamu ya Fidyah iliopo Zariya na Huseinia ya mashia wa Saminaka imebolewa na viongozi wa serikali ya Kadona na majeshi ya nchi hiyo.
Shule hiyo ilisajiliwa na taasisi ya harakati ya Kiislamu Nigeria, ilikuwa inafundisha wanafunzi wa chekechea, msingi na Sekondari, ambapo ilikuwa ina mamia ya wanafunzi wa kiislamu katika shule hiyo.
Huseinia ya wafuasi wa madhehebu ya AhlulBayt (a.s) iliokuwa bado haujakamilika ujenzi wake pia imeharibiwa na viongozi wa jimbo hilo.
Watekelezaji wa amri ya serikali hiyo, kabla ya hapo hawakuwa wenyekutoa tangazo lolote kuhusu suala hilo, pia walipokuwa wamefika kwaajili ya kuharibu hawakuonyesha hukumu ya mahakama inayoashiaria kutoa hukumu hiyo, bali walikuja na vifaa vya kubomoa huku wakiwa na majeshi ambayo yamejianda kikamilifu wakiwa na silaha nzito za kila aina na kuharibu sehemu hiyo.
Katika hali ya kuharibu shule hiyo, pia wameharibu kaburi la Haji Hamid ambaye alizikwa katika shule hiyo, huku ripoti zikiashiria kuibiwa kwa mali zote za thamani ziliokuwa katika shule hiyo.   

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky