Mpango wa Saudi Arabia wa kumuuwa Raisi wa Misri wafichuka

  • Habari NO : 793402
  • Rejea : ABNA
Brief

Mahakama kuu ya Misri yaeleza jaribio la serikali ya Saudi Arabia ya kutaka kumuuwa Abdel Fattah el-Sisi Rais wa jamhuri ya Misri

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mahakama kuu ya Misri imetangaza habari hiyo siku ya Jumapili na kutoa kauli ya kugundua na kusambaratisha mitego miwili iliokuwa imetegwa kwaaji ya mauaji ya Abdel Fattah el Sisi ambaye ni Rais wa jamhuri ya Misri katika mji mtukufu wa Makkah.
Kwa mujibu wa ripoti hii, moja kati ya mpango wa mauaji hayo yalipangwa nchini Saudi Arabia, ambapo ilipangwa kuwepo na kikundi ambacho kitafanya mauaji hayo, katika kipindi ambacho Rais huyo atakapokuwa akifanya ibada ya Umra katika mji mtukufu wa Makkah.
Kikundi kilichopangwa kufanya mauaji hayo kilipangwa katika jengo lenye mnara wa saa katika Masjidul Haram, ambapo walikuwa ni wafanyakazi wa hoteli hiyo ambayo ilipangwa Rais huyo kukaa katika sehemu hiyo, waliopangwa kufanya shambulio hilo waliandaa vifaa vya kutengeza bomu, na kufanikiwa kulitengeza na kulitega katika moja ya majengo yaliopo katika Hoteli hiyo ili kuripua Hoteli hiyo na kumuuwa Rais huyo.
Aidha ilipangwa kwamba mmoja kati ya waliopangwa kufanya mauaji hayo, ajivishe mkanda wa mabomu na kujiripua katika jengo liliokuwa na mnara wa Saa ili kukamilisha shambulio hilo na kumsambaratisha Rais huyo.
Jaribio lingine la kumuuwa Rais wa Misri limegunduliwa ndani ya nchi ya Misri, ambapo wanajeshi kadhaa wa usalama nchini humo, ambao walikuwa na fikra ya kikundi cha kigaidi cha Daesh walipanga kufanya tukio hilo la kumuuwa Rais huyo ambapo pia halikuweza kufikia tija yake.

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky