janga la Mina na ziara ya Karbala

Kutoka Mina mpaka Karbala.... fedheha kwa Saudi Arabia adhama na utukufu kwa Iraq

  • Habari NO : 794532
  • Rejea : ABNA
Brief

Shirika la habari la Mesr Times lashindanisha aina ya ufanyaji wa maadhimisho ya arubaini ya Imam Husaein katika mji wa Karbala na ufanyikaji wa maadhimisho ya ibada ya Hija nchini Saudi Arabia kwa mtazamo wa wananchi wa Misri.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: shirika la habari la Mesr Times limenukuu makala ilioandikwa na Umniyat Fuadi akisema: wananchi wa Misri baada ya kuona picha za mamilioni ya watu waliomzuru mjukuu wa Mtume k(a.s) katika mji wa Karbala, walianza kulinganisha wingi wa watu hao na janga la kusikitisha liliotokea Mina ... na kusababisha vifo vya maelfu ya waislamu, huku wakijiuliza kwamba, mbona hatujasikia kuuwawa kwa watu kutokana na msongamano huo mkubwa wa karbala?, pia Pamoja na kuwepo ushahidi wakutosha unaonyesha uzembe wa serikali ya Saudia katika sehemu takatifu za Makka na Madina, Kwanini serikali ya Saudi Arabia inalazimisha watu waamini kuwa matukio ya Mina mengineyo kuwa ni yakawaida?
Aidha mwandishi aliendelea kwa kusema: hivi mwafahamu:
Saudia: mahujaji wakiwa zaidi ya milioni mbili ndani ya nchi yao, hunyongea na kutoridhishwa!
Iraq : wanaozuru siku ya arubaini, kama watapungua chini ya milioni 20, hawajihisi vizuri na kusikitika!
Saudia: kusimamizi mahujaji milioni mbili, hutengeza wizara maalumu!
Iraq : Maukib moja inaweza kusimamia wanaozuru milioni 8 bila tatizo!
Saudia: katika kila huduma wanayotoa kwa mahujaji huchukua pesa
Iraq: huduma zote kwa kipindi chote cha maadhimisho ni bure!
Saudia: hija kwao ni msimu wa kuchuma!
Iraq: muda wa ziara kwao ni muda wa kutoa na kukirimu!
Saudia: mahujaji milioni mbili husababisha foleni nakufungwa barabara!
Iraq: watu milioni mbili, ni idadi ya kawaida, hutosha barabara ndogo zaidi ya Karbala!
Saudia: wafalme na viongozi hutekeleza ibada ya Hija na magari ya kifahali!
 Iraq: viongozi na wananchi kwa pamoja bila ya viatu humzuru mjukuu wa Mtume (s.a.w.w)!
Saudia: huchukua pesa nyingi kwa mahujaji, hapohapo hujikweza na kujioa wamefanya jambo kubwa!
Iraq: wafanya ziara huombwa msamaha kwa mapungufu yasiokuwa ya makusudi!
Saudia: barabara moja kuingia mahujaji elfu 10, inasababisha mbano na vifo vya mahujaji!
Iraq: kama barabara moja ikawa na mazuwari milioni tautu, msimamizi wa maukibu huangalia barabara nakusema: barabara haina watu, wakowapi mazuwari wa Husein (a.s)!?
Saudia: nyumba ya mwenyezi Mungu (kaaba) ni kwaajili ya mawahabi pekee!
Iraq: Imam Husein (a.s) ni kwaajili ya wote!
Aidha Shirika la habari Mesrtimes linaendelea kusema: Shirika la habari la Ufaransa, limesambaza picha zinazoonyesha wengi wa watu waliokwenda katika arubaini ya Imam Husein (a.s) na kuandika kuwa waislamu wanaazimisha msafara wa watoto na familia ya Imam Husein (a.s) aliouliwa kikatili mnamo mwaka wa 61 A.H, katika ardhi ya Karbala, ambapo waislamu hao hutembea masafa marefu kwa muda wa siku 40, ambapo katika baadhi ya maeneo hutembea umbali wa zaidi ya kilometa miamoja wakiwa na famolia zao, nk

mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky