Saudia: mahusiano mazuri na Misri hayatakuwa mpaka ajiuzuru wazir wa mambo ya nje wa Misri

  • Habari NO : 795076
  • Rejea : ABNA
Brief

Serikali ya Riyadh yasema kuwa kukutana katika ya waziri wa mambo ya nje wa Iran na Misri, ni sawa na kukabiliana kwa maficho na serikali ya Saudia na kuanza fungamano jipya baina ya serikali ya Cairo na Teheran, ambapo kuonana huku kumepelekea Saudi Arabia kukasirika vikali huku ikitoa sharti la kwamba kama Misri itataka kurudisha uhusiano wake na Saudi Arabia, lazima ajiuzulu waziri wa mambo ya nje wa Misri Samih Shukriy

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Serikali ya Saudi Arabia imetangaza kuwa halitakuwa na fungamano la kawaida mpaka atakapojiuzulu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Arabi21 ni kwamba; ushahidi unaonyesha kuwa waziri wa mambo ya nje wa Misri ni katika wale ambao wana azma ya kuhoisha fungamano la Misri na Saudi Arabia, huku serikali ya Saudi Arabia ikiamini kuwa waziri huyo ndio chanzo cha hitilafu baina ya serikali ya Riyadh na Cairo.
Kukutana kwa Samih Shukriy (waziri wa mambo ya nje wa Misri) na Muhammad Jawadi Zarif (waziri wa mambo ya nje wa Iran) nje ya kikao cha mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa, ni ishara ya kupingana kwa waziri huyo na fikra potovu za kiwahabi, ambapo waziri huyo aliipinga kwa wazi siasa mbaya ya Saudi Arabi na kusema kuwa Saudia ndiye mzalishaji mkubwa wa magaidi, jambo ambalo limepelekea serikali ya Saudi Arabia kukasirishwa na msimamo wake huo hatimaye kutoa masharti hayo.
Vyanzo vya kidiplomasia vimetangaza kuwa: serikali ya Cairo imepinga vikali matakwa ya serikali ya Saudi Arabia ya kutaka kujiuzulu kwa waziri huyo, huku ikisisitiza kuwa suala hilo ni lakitaifa na hapaswi yeyeto wa nje ya taifa hilo kuingilia.
Mmoja kati ya wahalili wa Misri amesema kuwa maamuzi ya waziri wa mambo ya nje wa Misri, hayakuwa maamuzi binafsi, bali ni maamuzi ya wizara yake ambayo yako rasmi kwa mujiu wa serikali ya Raisi wa nchi hiyo, ambapo kwa kujiuzulu kwake hakutasaidia lolote.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky