Mahakama kuu ya Nigeria yatoa hukumu ya kuachiwa huru Sheikh Zakizakiy na mkewe

  • Habari NO : 795624
  • Rejea : ABNA
Brief

Mahakama kuu ya serikali ya Nigeria leo imetoa hukumu ya kuachiwa huru Sheikh Ibrahim Zakizakiy na familia yake haraka iwezekanavyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: moja kati ya matawi ya mahakama kuu ya Nigeria katika mji wa Abuja, imetoa hukumu hiyo leo hii inayoashiria kuwachiwa huru hara sheikh Ibrahim Zakizakiy.
Mahakama hiyo imebainisha kuwa: suala la kukamatwa kwa Sheikh Ibrahim Zakizakiy likuwa ni kinyume na sheria, jmabo liliopelekea mahakam hiyo kutoa amri ya kuachiwa huru sheikh huyo haraka iwezekanavyo.
Hakimu wa mahakama hiyo ametoa hukumu hiyo: serikali ya Nigeria inalazimika kumuacha huru sheikh huyo na familia yake ndani ya muda wa siku 45, na kuwakabidhi jeshi la polisi la nchi hiyo na kwenda kumweka katika moja ya sehemu ziliokuwa na amani nchini humo.
Hakimu huyo amedai kuwa sababu ziliotolewa na vyombo vya usalama wa nchi hiyo  ni sababu butu ambazo hazifai kuzingatiwa, huku akiendelea kusema kuwa, kuendelea kuwekwa kwake kizimbani ni jambo lilio kinyume na sheria ya nchi hiyo.
Aidha amesema, mpaka sasa mahaka haijapata mashtaka yoyote kutoka kwa wananchi wanaoishi katika eneo aliokuwa anaishi sheikh huyo, mashtaka ambayo yanayoonyesha kuudhiwa na harakati za kiongozi huyo wa kidini nchini Nigeria.
Hakimu wa mahakama pia ameashiria hali ya afya aliokuwanayo Sheikh huyo nakusema kuwa: kunauwezekano mkubwa wa kutokea machafuko makubwa nchini humo endapo kiongozi huyo atafariki, machafuko ambayo yatapelekea kuuwawa wananchi wengi wasiokuwa na hatia.
Kwa mujibu wa hukumu ya mahakama, mahakama imetoa siku 45 za kuachiwa sheikh huyo na familia yake na kukabidhiwa jeshi la Polisi, amapo jeshi la polisi litakuwa na masaa 24 ya kumfikisha sheikh na familia yake katika sehemu ya amani na usalama.
Mahakama emeilazimisha idara ya ulinzi ya Nigeria itoe kiasi cha pesa milioni 50 ya kinigeria ambayo ni sawa na dola 160000 za kimarekani kwa familia ya sheikh Ibrahim Zakizakiy.
mwisho/290


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky