Watu 60 wauwawa na kujeruhiwa kufuatia mripuko wa kigaidi mkabala na kanisa mjini Cairo+ picha

  • Habari NO : 797514
  • Rejea : ABNA
Brief

Kwa uchache watu 25 wameuwawa Kufuatia mripuko wa kigaidi uliotokea mkabala na kanisa mjini Cairo Misri

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya afya nchini Misri imetangaza kwamba: mpaka sasa kwa uchache watu 25 kuuwawa na 35 kujeruhiwa kufuatia mripuko ulitokea mkabala na kanisa la waqibti sehemu ya Abbasia mjini Cairo.
Majeshi ya uokozi na usalama wa taifa yamefika katika sehemu ya tukio ili kuchunguza chanzo cha tukio hilo, aidha Rais wa jamhuri ya Misri ametoa siku tatu za maombolezo kufuatia tukio hilo katika maeneo malimbali ya taifa hlo.
Mripuko huo umetokea katika hali ambayo siku ya Ijumaa pia kulitokea na mripuko wa kigaidi katika mkoa wa Al-Jaizah na kusababisha vifo vya wanajeshi 6 wa usala na wengine 3 kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa ripoti hii inasemekana kuwa kikundi cha kigaidi cha Misri kinachoitwa “Sawaidu Misri” ndio kilichotangaza kuhusika na shambulio hilo la Ijumaa.
Kikundi hicho kimetoa kauli na kusema kuwa: wao ndio walio fanya shambulizi la sehemu ya mkusanyiko wa majeshi ya nchi hiyo, katika barabara ya Alharamu Al Jaizah kwakutega bomu la kutengaa kwa mikono, ambapo kufuatia shambulio hilo wanajeshi 6 wa nchi hiyo walipoteza maisha na wanajeshi wengine watatu kujeruhiwa vibaya.
mwisho/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky