Obama awafukuza wawakilishi Urusi, Marekani

  • Habari NO : 801770
  • Rejea : abna.ir
Brief

Rais wa Marekani Barack Obama ameamuru kufukuzwa maafisa 35 wa Urusi na kuyawekea vikwazo mashirika ya ujasusi ya Urusi kufuatia madai ya udukuzi wa mitandao ya taasisi za kisiasa katika uchaguzi mkuu wa Marekani, ambapo mgombea wa chama cha Obama ambaye alikuwa akisaidiwa na vyombo vya habari aliangushwa na Trump kupata ushindi mkubwa, baada ya ushindi huo serikali ya Obama ilidai kuwa Urusi ndo ilisababisha ushindi wa Trump.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Marekani Barack Obama ameamuru kufukuzwa maafisa 35 wa Urusi na kuyawekea vikwazo mashirika ya ujasusi ya Urusi kufuatia madai ya udukuzi wa mitandao ya taasisi za kisiasa katika uchaguzi mkuu wa Marekani, ambapo mgombea wa chama cha Obama ambaye alikuwa akisaidiwa na vyombo vya habari aliangushwa na Trump kupata ushindi mkubwa, baada ya ushindi huo serikali ya Obama ilidai kuwa Urusi ndo ilisababisha ushindi wa Trump.

Hatua hizo zilizochukuliwa katika siku za mwisho wa utawala wa Obama, zinaashiria kiwango kipya cha chini kabisaa katika uhusiano wa Marekani na Urusi baada ya vita baridi, na zimeweka uwezekano wa mvutano kati ya rais ajaye Donald Trump na Warepublican wenzake wanaodhibiti bunge la Congress, juu ya namna ya kuishughulikia Urusi.

Obama ambaye ni kutoka chama cha Democratic, aliahidi kuchukuwa hatua baada ya maafisa wa uchunguzi kuilaumu Urusi kwa udukuzi uliolenga kushawishi matokeo ya uchaguzi wa rais. Maafisa walimnyoonshea kidole moja kwa moja rais Vladmir Putin kwa kuongoza binafsi udukuzi huo, ukiwalenga hasa wanasiasa wa chama cha Democratic, ambao walimtia kishindo Obama kuchukuwa hatua, baada ya kushindwa vikali katika uchaguzi huo.

"Hatua hizo zinafutia onyo za siri na za wazi tulizozitoa mara kwa mara kwa serikali ya Urusi, na ndiyo majibu stahiki dhidi ya juhudi za kuhatarisha maslahi ya Marekani kwa kukiuka utaratibu uliowekwa kimataifa," Obama alisema katika taarifa kutoka mapumzikoni mjini Hawaii, na kuongeza kuwa Wamarekani wote wanapaswa kustushwa na vitendo vya Urusi. Obama na chama chake wanataka kuwapoza wanachama wao kwa kusingizia kuwa Urusi ilingilia na kubadili matokea ya Uchaguzi na kwamba chama cha Obama ndio kilikuwa kimeshinda uchaguzi huo uliokuwa na mvutano mkali, huku viongozi wote wa Ulaya wakiitetea chama cha Obama na kumponda Trump, ambapo walipata mshtuko kubwa baada ya Trump kuwa mshindi wa uchaguzi.

Wanadiplomasia wa Urusi wapewa siku 3 kuondoka Marekani

Obama alisema Warusi hawataruhusiwa kuyatumia tena majengo mawili yanayomilikiwa na serikali ya Urusi yalioko Maryland na New York na serikali imetoa muda wa siku tatu  kwa maafisa wa Urusi waliotuhumiwa kuondoka marekani pamoja na familia zao. Mashirika ya Ujasusi ya Marekani yamehitimisha kwamba  lengo la Urusi lilikuwa kumsaidia Donald Trump kushinda uchaguzi  madai  ambayo Trump ameipinga kama kichekesho, madai hayo pia yanamchekesha kila mtu mwenye kujua siasa za uchaguzi wa Marekani.

Na haijabainika wazi iwapo Trump, ambaye amemsifu Putin mara kwa mara, na kuwateuwa watu wanaoonekana kama marafiki wa serikali ya Moscow katika nyadhifa za juu serikalini, atataka kufuta hatua hizo pale atakapochukuwa madaraka Januari 20. Trump hata hivyo alisema siku ya Alhamisi kuwa angekutana na maafisa wa idara za ujasusi kupata maelezo zaidi.

Wabunge wa vyama vya Democratic na Republican wameelezea wasiwasi juu ya vitendo vya Urusi, na hivyo kuweka uwezekano wa upinzani iwapo Trump atajaribu kuondoa hatua hizo. Spika wa baraza la wawakilishi Mrepublican Paul Ryan, alisema Urusi imekuwa ikitaka kudhoofisha maslahi ya Marekani na kusema vikwazo hivyo vimechelewa. Maseneta wa chama cha Republican John McCain na Lindsay Grahama, walisema wanakusudia kuongoza juhudi bungeni kuiwekea Urusi vikwazo vikali zaidi.

"Nina wasiwasi juu ya nini kitatokea nchini Ufaransa, Ujerumani kuhusiana na ushiriki wa Urusi. Lakini tunahitaji kuweka msimamo, na hilo litahitaji maumivu kidogo. Vikwazo tunavyovitaka vitakuwa vya kidukizi zaidi kuliko vya sasa. Vitaiumiza Urusi zaidi," alisema Graham akijaribu kushawishi watu katika mkutano na waandishi wa habari.

Urusi yaahidi kujibu kwa kutumia hekima

Ikulu ya Kremlin ambayo imelaani vikwazo hivyo na kuvitaja kuwa kinyume cha sheria na kuahidi kujibu ipasavyo, imehoji iwapo Trump ataidhinisha vikwazo hivyo vipya.  Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov ameutuhumu utawala wa Obama kwa kujaribu kuharibu kabisaa uhusiano wa Marekani na Urusi, na kuahidi Moscow itajibu vile inavyostahiki.

Maafisa wa Marekani wamesema wana taarifa kwamba Urusi imeifunga shule ya Anglo-Amerika katika mji mkuu Moscow, ambayo inahudhuriwa zaidi na watoto wa wanadiplomasia, lakini hawakuweza kuthibitisha ripoti hizo.

Trump amehoji iwapo kweli Urusi ilibadili mwelekeo wa matokeo, akizikosoa tuhuma za Obama kama juhudi za Rais wa chama cha Democratic kuharamisha ushindi wa Mrepublican. Wakati tayari Trump amepokea taarifa za kiintelijensia kuhusu uchaguzi na ushahidi wa kutosha umewekwa hadharani, ahadi yake ya kukutana na wakuu wa mashirika ya ujasusi inaweza kutoa fursa ya kulegeza msimamo wake.

Rais Barak Obama kwa sasa anaondoka madarakani huku ameishusha Marekani katika nyanja mbali mbali na kuifanya Marekani ambayo ilikuwa ikisifika kama nchi kubwa duniani kuwa chini ya Urusi na China na bado inaendelea kushirikiana na mataifa ya kiarabu katika kusaidia magaidi nchini Syria na Iraq.

Mwisho wa habari / 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

We are All Zakzaky