Majibu ya Urusi kuhusu kufukuzwa wawakilishi wake yamshusha Obama

  • Habari NO : 801771
  • Rejea : abna.ir
Brief

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameijibu Marekani kwa kuahidi kutowafukuza wawakilishi wa Marekani kama alivyofanya Obama na badala yake itatumia njia za hekima, hatua hii imeonekana kuonyesha upeo wa hali ya juu ya Putin katika uongozi na Siasa, huku ikimshusha Obama kwa kushawishiwa na kukurupuka kutoa maamuzi mazito ili kuharibu uongozi wa rais Trump ambaye anatarajiwa kuiongoza Marekani kwanzia januari 20.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais Vladimir Putin wa Urusi ameijibu Marekani kwa kuahidi kutowafukuza wawakilishi wa Marekani kama alivyofanya Obama na badala yake itatumia njia za hekima, hatua hii imeonekana kuonyesha upeo wa hali ya juu ya Putin katika uongozi na Siasa, huku ikimshusha Obama kwa kushawishiwa na kukurupuka kutoa maamuzi mazito ili kuharibu uongozi wa rais Trump ambaye anatarajiwa kuiongoza Marekani kwanzia januari 20.

Shirika la habari la RIA limemnukuu rais Vladimir Putin akisema atazingatia hatua zitakazochukuliwa na rais mteule Donald Trump atakaekabidhiwa hatamu za uongozi january 20 mwakani, kabla ya kupitisha hatua ziada kuhusu uhusiano kati ya Urusi na Marekani.

Hapo awali waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lavrow alimshauri rais Putin aamuru serikali ya mjini Moscow iwafukuze wanadiplomasia 35 wa Marekani na kuwazuwia wanadiplomasia hao wa Marekani kutumia majengo mawili yaliyoko mjini Moscow. Lakini upevu na hekima za Putin zimezuia hatua hiyo na kumfanya Obama kuonekana kichekesho mbele ya jamii, ambapo kwasasa nchi nyingi zinajitahidi kutafuta Marafiki lakini Obama anataka kufukuza marafiki ili aharibu uongozi wa Trump.

Hayo yamesababishwa na uamuzi wa rais Barack Obama wa kuwafukuza wanadiplomsia 35 wa Urusi wanaotuhumiwa kufanya upelelezi pamoja na kuyawekea vikwazo mashirika mawili ya upelelezi ya Urusi kwa tuhuma kwamba yamehusika katika udukuzi dhidi ya makundi ya kisiasa katika uchaguzi wa rais mwaka huu. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi, Sergei Lavrov amezitaja tuhuma kwamba Urusi imeingilia kati katika uchaguzi wa Marekani kuwa "hazina msingi."

Hakuna kiongozi yeyote wa Marekani atakaefukuzwa-anasema Vladimir Putin

Rais Vladimir Putin amelikataa pendekezo la waziri wake wa mambo ya nchi za nje:"Hatutomfukuza yeyote" amesema rais Putin katika taarifa yake. Ameongeza kusema pia kwamba anaviangalia vikwazo ziada kuwa sawa na hatua nyengine ya kuvuruga uhusiano kati ya serikali yake na serikali ijayo ya Trump. Amesema anasikitika kuona serikali ya Obama inamaliza mhula wake  kwa ubaya namna hiyo.

Maafisa wa Urusi wamevitaja vikwazo vya Marekani kuwa hatua ya mwisho ya rais aliyedhoofika na kuashiria uwezekano wa kumuona rais mteule Donald Trump akibadilisha mkondo wa mambo atakapokabidhiwa hatamu za uongozi january 20 mwaka kesho.

Hata hivyo wanachama kadhaa wa Republican hawavutiwi na fikra ya kuwepo usuhuba pamoja na Urusi na badala yake wanaunga mkono vikwazo dhidi ya Moscow. John McCain na Lindsey Graham, vigogo katika baraza la Senet, wameshasema watahakikisha vikwazo vikali zaidi vinawekwa dhidi ya Urusi ambayo kwasasa imeizidi nguvu Marekani katika sekta mbali mbali na kuifanya Marekani kuwa dhoofu kila kukicha.

"Hatua za mwenye uchungu wa kukata roho" wanasema maafisa wa serikali ya Urusi

"Inasikitisha kwamba serikali ya Obama iliyoanza kwa kurejesha mshikamano kati ya nchi zetu, inamaliza mhula wake kwa "uchungu wa kukata roho." amesema Dmitry Medvedev aliyewahi kuwa waziri mkuu mnamo mwaka 2009 na kusaidia pale rais Barack Obama alipoanza juhudi za kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Urusi.

Wakati huo huo wizara ya mambo ya nchi za nje ya Urusi imekanusha ripoti za vyombo vya habari zinazodai kwamba maafisa wa serikali wameamuru shule ya kimarekani iliyoko mjini Moscow ifungwe.

Rais Putin amekuwa akitumia hekima ya hali ya juu katika kutatua matatizo ambao hata tukuo la kuuawa Balozi wa Urusi nchini Uturuki lina nasibishwa kuwa linatokana na uchochezi wa Marekani ili kuvuruga uhusiano wa Uturuki na Urusi lakin Putin hakuonyesha kuhamaki wala kutangaza kisasi dhidi ya hujuma hiyo ya kinyama.

Mwisho wa habari/ 291

 

 


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Mourining of Imam Hossein
پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1440 / 2019
We are All Zakzaky