Jina la Hashemi Rafsanjani daima huambatana na la Imam Khumeini na mapinduzi ya kiislam ya Iran

  • Habari NO : 803874
  • Rejea : ABNA
Brief

Jumuia ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s) yatoa kauli na rambirambi kufuatia kufariki kwa “Ayatullah Hashemi Rafsanjani” mfuasi wakaribu wa Imam Khumeini na kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jumuia ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s) imetoa ujumbe wa rambirambi kufuatia kufariki kwa “Ayatullah Hashemi Rafsanjani miongoni mwa watu wakaribu kwa Imam Khumeini na kiongozi wa mapenduzi ya kiislamu ya Iran Sayyed Ali Khamenei.
Ujumbe huu ni kama ifuatavyo:
Kwajina la mwenyezi Mungu mwingi wa rehama mwenye kurehemu
مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَ مِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَ مَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً
 Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha( ahadi )hata kidogo(Ahzab:23)
Tumepokea habari za kusikitisha za kufariki kwa Ayatullah Akbar Hashemi Rafsanjani, mpambanaji mkubwa kutoka mwanzo wa mapinduzi ya kiislamu mpaka mwisho wa uhai wake, ambaye ni mtu wa karibu sana kwa Imam Khumeiniy pia mshirika wa karibu na kiongozi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran “Ayatullah Sayyed Ali Khamenei” katika vita ya miaka minane ya mapinduzi ya kiislamu ya Iran.
Kifo chake kimeambatana na tarehe 19 dey kwa mwezi wa kiiran ambao unasadifiana na siku ambayo waumini wa mji wa Qum wasimama dhidi ya utawala wa kifalme wa Shaha, hivyo imesadifiana na mnasaba mzuri na kifo cha mpambanaji huyo mkongwe katika tarehe ya Iran ya kiislam.
Ushujaa wa mkongwe huyu katika miaka aliokuwa amefungwa na kuamishwa kupelekwa kwake sehemu mbalimbali, kulikuwa kunatokana na kusisitiza kwake kuhusu ushindi wa Imam Khumeini katika nyakati nzito za vitisho vya utawala wa mfalme Shaha wa Iran, aidha alikuwa ni mtu wa kwanza kuyahami mataifa dhaifu kama vile Palestinana Lebananon, bila ya kusahau juhudi zake katika kusimika misingi ya serikali ya kiislamu ya Iran, kukabiliana na fikira potovu za kinafiki, kutoa ushirikiano wake katika vita ya kujitetea ya miaka minane, uwezo wake wa kubainisha mambo katika hutuba za sala ya Ijumaa ambazo zilikuwa zikituliza nyoyo za waumini na juhudi zingine alizozifanya katika kupangilia serikali ya mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, hayo yote yamelifanya jina la Ayatullah Hashemi Rafsanjani kuwambatana na jina la Imam Khumeiniy na mapinduzi ya kiislamu ya Iran.
Ukiachana na mapambano yake ya kisiasa, marehemu alikuwa akijishughulisha na masuala ya kielimu na tafsiri, na kuwasaidia masikini na wenye kipato kichache ni miongoni mwa harakati za mwanazuoni huyu mkubwa.
Ama kuhusu fungamano na mtume Muhammad (s.a.w.w) na kizazi chake kitakatifu (a.s) imethibiti hali hayo katika hutuba zake, ambapo ni katika moja ya sehemu muhimu za maisha yake. Juhudi zake za kupunguza hali ya kuzuiliwa watu kwenda kuzuru katika makaburi ya Baqii ni katika tija ya juhudi zake, pia ikiwemo picha zake zinazoonyesha alipokuwa katika shamba la “Fadak fatimiy” ni katika ushuhuda wa upendo wake kwa kizazi cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Tunatoa rambirambi kwa Imam wa zama hizi (a.f), kiongozi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, viongozi wakuu wa dini, viuo vikuu vya dini, wapenda wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na wafiwa wote, pia tunawatakia kuwa na subra na ustahamilivu bila ya kusahau kumuombea maghfira na msamaha kwa mwenyezi  Mungu msamehevu.


Jumuia ya kumataifa ya
AhlulBayt (a.s) 8/1/2017


Tunapenda kukumbusha kuwa Ayatullah Hashemi Rafsanjani magharibi mwa siku ya Jumapili tarehe 8/1/2017 alipatwa na mstuko wa moyo hatimaye kupelekwa huspitali na baada ya muda kuaga dunia. Mwenyezi mungu aiweke pema roho ya marehemu, amin.

mwisho wa habari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni