Trump aishutumu Iran kwa majaribio ya makombora

  • Habari NO : 809070
  • Rejea : abna.ir
Brief

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Iran imewekwa katika "ilani" baada ya jaribio la karibuni la kombora, na kudai kwamba nchi hiyo ilikuwa kwenye kingo za kuporomoka kiuchumi wakati iliposaini makubaliano ya nyuklia.

Shirika la habari la ABNA inaripoti kuwa: Rais wa Marekani Donald Trump amesema Iran imewekwa katika "ilani" baada ya jaribio la karibuni la kombora, na kudai kwamba nchi hiyo ilikuwa kwenye kingo za kuporomoka kiuchumi wakati iliposaini makubaliano ya nyuklia.

Akirejea matamashi sawa na yaliotolewa na mshauri wake wa masuala ya usalama Michael Flynn siku moja kabla, Trump aliandika kwenye ukurasa wake twita mapema leo kwamba: "Iran imewekwa rasmi kwenye tahadhari kwa kufyatua kombora la masafa marefu. Ilipaswa kuwa na shukrani kwa makubaliano mabaya Marekani iliosaini nao!".

Wakati huo Iran imesisitiza kwamba nchi yeyote haina haki ya kuichagulia Iran kitu cha kufanya, na kwamba Iran ni taifa huru na lenye nguvu.

Lakini ikulu ya White House haijatoa ufafanuzi wa nini hasa maana ya onyo hilo kivitendo, na bado haijajulikana iwapo ikulu hiyo itataka kuiwekea Iran vikwazo safari hii. Flynn alisisitiza kwamba jaribio hilo la kombora lililofanyika siku ya Jumapili lilikuwa ukiukaji wa azimio la Umoja wa Mataifa nambari 2231, linaloitaka Iran kutojaribisha makombora yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.

Makombora ya Iran yanasadikiwa kuwa ni hatari kwa Israel ambayo mara kadhaa imekuwa ikiichokoza Iran na kujificha nyuma ya Marekani.

Maafisa wa jeshi la Iran wamesema kuwa Iran ina mfumo wa makombora ya kuiangamiza Israel katika kipindi kisichozidi dakika saba, na pia wanauwezo wa kushambulia na kuangamiza  kambi zote za Marekani zilizo mashariki ya kati.

Madai ya kuwa Iran si sahihi

Trump na Flynn wamekuwa wakosoaji wakubwa wa serikali ya mjini Tehran na wapinzani wa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na mataifa makubwa, yaliopelekea Iran kuzuia mpango wake wa nyuklia na badala yake ikalegezewa vikwazo. Trump alisema katika tweet yake ya pili alfajiri kwamba Iran ilikuwa hoi ikisubiri tu kuporomoka, wakati Marekani ilipokuja kuinusuru kupitia makubaliano hayo yalioihakikishia kiasi cha dola bilioni 150 katika kulegezewa vikwazo.

Serikali ya Obama ndio iliyoomba umoja wa mataifa kuweka vikao vya sulhu kuhusu mpango wa nyuklia ya Iran, viongozi wa Iran wamesisitiza kuwa hawatishi na vikwazo kwani wamekuwa katika vikwazo kwa takriban miaka 30.

mshauri wa juu wa kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alisema siku ya Alhamisi kuwa Iran haiwezi kutishwa na kauli za vitisho za Marekani kuhusiana na jaribio lake la kombora zinazotolewa na rais asiyekuwa na uzoefu wowote katika uongozi. Iran ilikiri jana kuwa ilifanya jaribio la kombora hilo lakini ikasema jaribio hilo halikukiuka makubaliano kati yake na mataifa sita makubwa, au azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Mshauri huyo wa Khamenei  Ali Akbar Velayati, alinukuliwa na shirika la habari la Fars akisema "hii siyo mara ya kwanza kwa mtu asie na uzowefu kuitishia Iran", na kuongeza kuwa serikali ya Trump hivi karibuni itafahamu kuwa kuitishia Iran hakuna faida yeyote. Afisa wa Marekani alisema kombora hilo la Iran lilisafiri umbali wa kilomita 1,010, madai ambayo Iran iliyakanusha.

sintofahamu kati ya Trump na waziri mkuu Australia

Wakati huo huo gazeti la Washington Post, likinukuu duru kutoka serikali ya Marekani, limeripoti kuwa Trump alimkaripia vibaya waziri mkuu wa Australia Malcom Turnbull wakati wa mazungumzo yao ya kwenye simu siku ya Jumapili, na kufikia hatua ya kumkatia simu kiongozi huyo wa taifa mshirika wa Marekani, kuhusiana na makubaliano juu ya Marekani kuwapokea wakimbizi waliokataliwa na Australia, ambao kwa mujibu wa makubaliano hayo yaliofikiwa wakati wa utawala wa Obama, Marekani inatakiwa kuwachukuwa.

Imeripotiwa kuwa Trump aliitaja simu aliompigia Turnbull kuwa mbaya zaidi kati ya simu nne aliozowapigia viongozi wa dunia siku hiyo.

Ingawa waziri mkuu Turnbull alisema mazungumzo kati yake ya Trump yalikuwa ya kirafiki, na kwamba rais huyo alikubali kuheshimu makubaliano hayo na pia msemaji wa White House Sean Spicer kuthibitisha hivyo, Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa twita na kuyashambulia vikali makubaliano hayo na kuyataja kuwa ya kijinga na kuahidi kuyapitia upya. Turnbull anakusha kuwa Trump alimkatia simu na kusema anasikitika kwamba mazungumzo yake na Trump yalivujishwa.

"Nimesikitishwa sana kwamba kumevujishwa kile kinachodaiwa kuwa mazungumzo yetu ya simu mjini Washington. Lakini nataka niseme kitu kimoja kuhusu suala hilo. Ripoti kwamba Rais Trump alikataa simu siyo sahihi. Simu hiyo ilimalizika vizuri na kulingana na mazunungumzo yenyewe, yalikuwa ya wazi na kirafiki. Nawakilisha maslahi ya Australia. Natoa hoja za Australia kwa nguvu na kushawishi kadiri niwezavyo, popote ninapokuwa."

Wasaidizi wa Trump hawaujui Umoja wa Ulaya

Mratibu wa serikali ya Ujerumani wa masuala ya mataifa ya Atlantic Jürgen Hardt, amesema watu wanaomzunguka trump wana ufahamu kidogo kuhusu Umoja wa Ulaya, na kwamba Ujerumani inapaswa kuelezea namna kanda hiyo kubwa zaidi ya kibiashara duniani inavyofanya kazi.

Akiongea baada kufanya mazungumzo na maafisa waandamizi katika ikulu ya White House, Hardt aliliambia gazeti la Der Tagessspiegel, kwamba inaonekana utawala mpya Marekani unalena kuwa mahusiano na taifa mmoja mmoja na Umoja wa Ulaya.

Mapema jarida la Marekani la World Trade Online liliripoti kwamba mataifa kadhaa ya Umoja wa Ulaya yalikataa maombi ya utawala wa trump kujadiliana nayo mmoja mmoja mikataba ya kibiashara.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni